loader
Dstv Habarileo  Mobile
TPA
Picha

Ujenzi wa Magomeni Kota wafikia asilimia 81

UJENZI wa nyumba zilizomo kwenye mradi wa wakazi 644 wa Magomeni Kota jijini Dar es Salaam, umefikia asilimia 81.

Hayo yalibainika katka ziara ya Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (ujenzi), Elias Mwakalinga alipotembelea mradi wa ujenzi wa nyumba hizo jana.

Mwakalinga alisema tayari serikali imemalizia kiasi cha Sh bilioni tisa zilizokuwa zimebaki kukamilisha ujenzi huo ili kuwapatia wakazi hao makazi bora na salama.

"Eneo hili lilikuwa na vijumba vingi vidogo vidogo vilipobomolewa ndipo serikali iliona wananchi wanaishi eneo lisiloeleweka wakawa kama wametapeliwa, baadaye serikali ikaamua kuchukua eneo hilo na kuamua wajengewe nyumba hapa," alisema Mwakalinga na kueleza kufurahia kasi ya ujenzi wa makazi hayo.

"Mradi huu ulichelewa kidogo kwa sababu ya fedha sasa hivi fedha zimetolewa hivyo hakuna sababu ya kisingizio cha kusema hawatamaliza kwa muda kwa wakati huu," alisema.

Awali Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Majengo Tanzania (TBA), Daud Kondoro alisema mradi huo ulianza kutekelezwa Oktoba 2016 ikiwa ni ahadi ya Rais John Mafufuli kwa wananchi hao  waliokuwa wakiishi kwenye nyumba za awali.

Kondoro alisema TBA ilifanya usanifu wa majengo matano, manne yana sakafu nane kila moja na moja lina sakafu tisa na kwamba, kila sakafu moja inabeba jumla ya kaya 16.

"Ubunifu wa ujenzi wa mradi huu umelenga kuzipatia makazi bora familia 644 za waliokuwa wakazi wa Magomeni Kota kwa gharama nafuu na kwa kuzingatia thamani ya fedha ikiwa pamoja na kuunganisha makazi hayo na miundombinu ya huduma muhimu kama vile maji safi, maji taka, umeme na zinginezo”alisema.

Kondoro alisema mradi huo unaogharamiwa na serikali kwa Sh bilioni 20 unatarajiwa kukamilika Januari mwakani.

"Ujenzi wa mradi huu ulianza Oktoba 2016 na ulitarajiwa kumalizika katika kipindi cha mwaka mmoja ambapo mradi ungekemilika Septemba 31, 2017…hata hivyo kutokana na changamoto mbalimbali zikiwemo za kifedha, mradi ulisimama kwa vipindi tofauti kuanzia mwaka 2017," alisema.

Alisema gharama za utekelezaji wa mradi huo hadi kufikia Oktoba mwaka huu zimefikia zaidi ya Sh bilioni 43.

Kondoro alisema katika mradi huo, wametengeneza kitega uchumi kwa ajili ya kuwasaidia wakazi hao na kuingiza fedha kwa wakala.

Alisema wakala unatambua kuwa ukamilishaji wa mradi huo utawanufaisha wakazi hao na kuboresha sura ya eneo la Magomeni tofauti na ilivyokuwa awali.

"Pia serikali itakuwa imetimiza azma yake kwa mujibu wa sera kuhakikisha wananchi hao wanakuwa na makazi bora," alisema Kondoro.

MSANII wa Bongo fl eva , Zuwena Mohammed ...

foto
Mwandishi: Lucy Ngowi

Post your comments

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi