loader
Dstv Habarileo  Mobile
TPA
Picha

Wazazi Mpunguzi watakiwa kuwawekea akiba watoto wao

WAZAZI na walezi wa Kata ya Mpunguzi Jiji la Dodoma wametakiwa kujenga mazoea ya kuwawekea akiba ya fedha na mali kwa ajili ya watoto wao katika kipindi chote wanaposoma shule za sekondari.

Wito huo umetolewa na Mkuu wa Chuo cha Mipango ya Maendeleo Vijijini, Profesa Hozen Mayaya.

Profesa Mayaya alisema hayo alipozungumza na wazazi, walezi wa kata hiyo kwenye mahafali ya kuwaaga wanafunzi waliohitimu darasa la saba mwaka huu.

Akizungumza kwa niaba yake, Mkuu wa Kitengo cha Masoko na Uhusiano wa Chuo hicho cha Mipango, Godrick Ngolly alisema kuwa kitendo cha kuwawekea akiba kitasaidia kuwalipia fedha wataapokuwa kidato cha tano na sita. Pia wale watakaojiunga na vyuo vikuu, watatumia akiba hiyo kulipia mahitaji.

Alisema ushahidi unaonekana kwa baadhi ya wazazi, walezi wenye watoto wanaosoma shule za sekondari na vyuo vikuu wanashindwa kuwaendeleza kielimu kutokana na fedha nyingi zinazohitaji kumlipia mwanafunzi.

"Suala la kujijengea tabia ya kujiwekea akiba liwe la utamaduni kwa kila mzazi na mlezi, hii itaweza kuwasaidia wanafunzi kusoma na kufikia ndoto ili aweze kulitumikia taifa kwa malengo ya kuleta maendeleo yao wenyewe, wazazi na taifa pia," Professa alisema.

Kwa upande wao, wanafunzi waliohitimu walitakiwa kutojihusisha kwenye makundi maovu, ambayo yanayoweza kuwakatisha ndoto walizokuwa nazo za kujiendeleza zaidi kielimu, kwa kuwa hatua waliyofikia si mwisho wa elimu yao.

Awali wakizungumza na waandishi wa habari kwenye mahafali hayo ya 62 tangu kuanzishwa shule hiyo mwaka 1952, wanafunzi hao waliwataka wazazi na walezi kuwaendeleza kielimu zaidi, badala ya kufikiria kuwatafutia kazi za majumbani na kuchunga  au wengine kuwaozesha.

Akizungumza kwa niaba ya wenzake, Jeremia Malugu alisema baadhi ya wazazi na walezi bado wana mtizamo hasi, ambao wamekuwa wakifikiria watoto wanaomaliza masomo tayari wanakuwa mitaji ndani ya familia zao kwa kuwatafutia vibarua vya kufanya na wengi kuwaonzesha, badala ya kuwaendeleza zaidi kielimu na hatimaye waweze kufikia ndoto zao.

Aliomba serikali kuanzia ngazi za mitaa hadi za juu, kuwachukulia hatua za kisheria wote wanaozimisha ndoto za wanafunzi, ambao wamekuwa wakitanguliza rushwa ili wasifikishwe kwenye vyombo vya kisheria.

MSANII wa Bongo fl eva , Zuwena Mohammed ...

foto
Mwandishi: Sifa Lubasi

Post your comments

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi