loader
Dstv Habarileo  Mobile
TPA
Picha

Mwanza waonywa rushwa Uchaguzi Mkuu

TAASISI ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) Mkoa wa Mwanza imeonya wagombea ubunge, udiwani na wananchi kutokutoa au kupokea rushwa wakati wa uchaguzi mkuu na itakuwa macho kudhibiti vitendo hivyo.

Mkuu wa Takukuru mkoani humo, Emmanuel Stenga alitoa onyo hilo wakati akitoa taarifa kuhusu utendaji wa taasisi hiyo Julai hadi Septemba mwaka huu.

"Wito kwa wananchi wa Mkoa wa Mwanza, wazingatie makatazo ya vitendo vya rushwa kwenye uchaguzi, kama mnavyofahamu huu ni uchaguzi wa Rais, wabunge na madiwani, wawe makini kwa kuepuka vitendo vya rushwa kabla, wakati na baada ya uchaguzi," alisema Stenga.

Aliomba wananchi waendelee kutoa ushirikiano kwa kutoa taarifa za vitendo hivyo ili Takukuru iwashughulikie wanaotoa na kupokea rushwa.

Stenga aliwaeleza waandishi wa habari kuwa katika kipindi hicho, imekagua miradi 16 ya maendeleo yenye thamani ya Sh 5,988,628,232.9 na Euro 6,891,021.08.

Alisema kati ya miradi hiyo, minane ni ya maji ambayo ina thamani ya Sh 4,432,947,136.84 na Euro 6,891,021.08.

Stenga alisema, miradi minne ni ya elimu yenye thamani ya Sh 648,702,556.06, miwili ya afya yenye thamani ya Sh 557,000,000, mmoja wa usafirishaji wenye thamani ya Sh 219,978,540 na mmoja wa ujenzi wa ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Kwimba wenye thamani ya Sh 130,000,000.

Alisema katika kipindi hicho, Takukuru ilipokea jumla ya taarifa 276 za vitendo vya rushwa na makosa mengine ya jinai.

Stenga alisema, kati ya taarifa zilizopokewa 48 zinahusu vyama vya siasa, 17- serikali za mitaa (wenyeviti wa vijiji, mitaa, vitongoji na kata), 35 taasisi za fedha, 25 ardhi, 23 idara ya elimu na 16 kutoka kampuni binafsi.

"Aidha katika kipindi hicho, jumla ya kesi mpya 9 zimefunguliwa, kesi 8 zimetolewa hukumu na kati ya hizo kesi 6 watuhumiwa wametiwa hatiani na kesi 23 zinaendelea mahakamani zikiwa katika hatua mbalimbali," alisema.

MKURUGENZI Mkuu wa Ofisi ya Takwimu ya Taifa (NBS), ...

foto
Mwandishi: Nashony Kennedy, Mwanza

Post your comments

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi