loader
Dstv Habarileo  Mobile
TPA
Picha

CHAMMUTA hawatumii neno kigugumizi kukwepa unyanyapaa

Mwenyekiti wa Chama cha Mtindo Maalum ya Uzungumzaji Tanzania (CHAMMUTA), Ally Abdallah amesema kuwa chama  hicho hakitumii neno kigugumimizi kwasababu kuna dhana potofu hapa nchini kuwa watu wa jamii hiyo wana ukosefu wa akili.

Abdallah amesema hayo jijini Dar es Salaam hii leo na kubainisha kuwa unyanyapaaji huo ndiyo uliwafanya kuachana na jina hilo ambalo limeharibiwa na kutafuta neno mbadala ambalo ni mtindo maalum wa uzungumzaji.

“ Watu wenye kigugumizi tuna wakati mgumu maana unaweza kuzungumza na mtu ambaye hana subira kwa kukukatisha unachotaka kusema pasipo kukusikiliza" amesema Abdallah.

Amesema kuwa kigugumizi sio ugonjwa ila kuna dhana tofauti hadi mtu kukipata ambapo kuna wanaosema kinatokana na kuzaliwa, huku wengine wakiamini mtoto akiwa mdogo  akimuona mtu mwenye kigugumizi naye akaiga hupata tatizo hilo, ambapo hivyo vyote bado vinafanyiwa utafiti kama vina ukweli wowote.

MKURUGENZI Mkuu wa Ofisi ya Takwimu ya Taifa (NBS), ...

foto
Mwandishi: Alfred Lukonge

Post your comments

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi