loader
Dstv Habarileo  Mobile
TPA
Picha

Homera: Mfumo mpya umeleta manufaa

Mkuu wa Mkoa wa Katavi, Juma Homera amesema kuwa kupitia Mfumo wa Stakabadhi Ghalani umesaidia wakulima wa mkoa huo kulipwa Tsh. Bilioni tano, mara baada ya kuuza ufuta kilo milioni 3.2 mwaka huu.

Homera amesema hayo  alipotembelewa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo Gerald Kusaya mkoani humo na kubainisha kuwa anafarijika kwa kiongozi huyo wa serikali kuwatembelea wakulima kwa lengo la kuwahamasisha kufanya kilimo cha kibiashara ili kujiongezea kipato.

Amesema kuwa  mafanikio hayo ya kukusanya Tsh. Bilioni tano kwa mwaka yalikumbana na changamoto nyingi ikiwemo baadhi ya viongozi wa ushirika wasiokuwa waadilifu kujaribu kuwanyima  wakulima stahiki zao.

Aidha, Homera alimpongeza Katibu Mkuu huyo kwa namna anavyotenga muda wake kufanya ziara katika maeneo mbalimbali ya nchi  ili kujionea ni namna gani changamoto mbalimbali zinazowakumba wakulima zinapatiwa ufumbuzi.

 Akizungumza katika tukio hilo Gerald Kusaya ambaye ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo amesema kuwa wizara imeanzisha mfumo wa ‘Mobile Utafiti’ wenye lengo la kufundisha maafisa ugani na wakulima nchini kuhusu namna bora ya kufanya kilimo cha kimkakati  ikiwemo Korosho.

“Natoa ahadi ya kuwaleta Katavi wataalam hao ili waje kutoa ujuzi ni namna gani wakulima wa mkoa huu wanaweza kujikita kwenye ulimaji wa zao la Korosho” amesema Kusaya.

MKURUGENZI Mkuu wa Ofisi ya Takwimu ya Taifa (NBS), ...

foto
Mwandishi: Alfred Lukonge

Post your comments

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi