loader
Dstv Habarileo  Mobile
TPA
Picha

Wananchi Kilimanjaro waombwa kumchagua Dk. Magufuli

Wananchi wa Wilaya ya Mwanga mkoani Kilimanjaro wameombwa kumchagua mgombea urais kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) John Magufuli  kwa kipindi cha miaka mingine mitano, kwakuwa ndiye mtu sahihi aliyeshika funguo ya wananchi wa hali ya chini katika kujipatia kipato bila bughudha kupitia shughuli zao za kujitafutia riziki.

Hayo yamesemwa na aliyekuwa Waziri Mkuu mara mbili kwenye Serikali ya  awamu ya kwanza na pili Cleopa Msuya kwenye mkutano wa kampeni wa mgombea huyo  wilayani  Mwanga mkoani Kilimanjaro mapema hii leo.

Msuya amesema kuwa kwa kipindi cha miaka mitano ya uongozi wake wananchi wameshuhudia mageuzi makubwa katika kila fani inayogusa wananchi wanyonge  kwa kuwafungulia milango kwa kila shughuli wanayofanya ya kuingiza kipato iwaletee manufaa.

Amewataka wananchi hao katika uchaguzi huu wathibitishe tena  kwa kumapa nafasi tena ya kushika kiti hicho ili pale alipoishia kwenye kuwainua wananchi wa hali ya chini aweze kumalizia.

Msuya alimshukuru mgombea huyo kwa kutoa ahadi ya kuushughulikia mradi wa maji kutoka Bwawa la Nyumba ya Mungu utakaonufaisha wananchi wa Wilaya hiyo wenye shida kubwa ya maji  pindi atakaporudi tena madarakani.

MSANII wa Bongo fl eva , Zuwena Mohammed ...

foto
Mwandishi: Alfred Lukonge

Post your comments

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi