loader
Dstv Habarileo  Mobile
TPA
Picha

JPM kukamilisha mradi Bwawa la Nyumba ya Mungu

Mgombea Urais kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) John Magufuli amesema kuwa iwapo atapata ridhaa ya wananchi kukalia kiti hicho kwa miaka mingine mitano atahakikisha  mradi wa maji kutoka Bwawa la Nyumba ya Mungu  hadi wilayani Mwanga unakamilika mara moja.

Magufuli amesema hayo muda mfupi uliopita alipokuwa wilayani Mwanga mkoani Kilimanjaro muda mfupi uliopita  kwenye muendelezo wa kampeni zake za kuwania tena kiti cha urais kwa miaka mingine mitano.

Amesema kuwa  kuwa mradi huo uliotakiwa ukamilike toka mwaka 2017 atausimamia yeye  mwenyewe kwakuwa ana uzoefu wa kutosha toka akiwa Waziri wa Ujenzi  ni namna gani ya  kuwabana wakandarasi  ili waweze kukamilisha miradi kwa wakati.

“Mradi huu unagharimu zaidi ya Tsh. bilioni 262 na ulitakiwa ukamilike miaka mitatu iliyopita,lakini wananchi wa eneo hili bado mnaendelea kupata shida ya maji  kutokana na kutokukamilika kwa wakati, natoa ahadi mkinichagua  jambo la kwanza nitahakikisha mradi huu ninausimamia mimi mwenyewe hadi utakapokamilika  ” amesema Magufuli.

Katika hatua nyingine alitoa ahadi kwa wakazi wa wilaya hiyo kukipandisha hadhi Kituo cha Afya cha Mwanga kuwa Hospitali ya Wilaya na kuwataka waache fikra mbaya ya kubaguana miongoni mwao kwa misingi ya ukabila kwakuwa wote ni watanzania.

 

 

 

MKURUGENZI Mkuu wa Ofisi ya Takwimu ya Taifa (NBS), ...

foto
Mwandishi: Alfred Lukonge

Post your comments

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi