loader
Dstv Habarileo  Mobile
Mradi wa maji Arusha kukamilishwa Desemba

Mradi wa maji Arusha kukamilishwa Desemba

Rais wa Tanzania Dk John Pombe Magufuli amemuagiza mkandarasi wa mradi wa maji jiji la Arusha ifikapo mwezi wa kumi na mbili mradi huo uwe umekamilika.

Dk Magufuli amesema hayo hii leo jijini Arusha na kumtaka mkandarasi huyo kuanza kufanya kazi usiku na mchana ili ifikapo mwezi wa kumi na mbili mradi huo uwe umekamilika.

Aidha,Dk Magufuli amesema kuwa mradi huo utakapokamilika utakuwa na uwezo kusambaza maji mara mbili ya mahitaji ya wakazi wa jiji hilo, hivyo mchakato utafanyika kupeleka maeneo jirani ya Hai, Simanjiro na Arumeru.

“Arusha ni jiji la kitalii ni aibu watu watoke nje wafike hapa wakose huduma ya maji” amesema DK Magufuli.

Vilevile Dk Magufuli aliwahakikishia wakazi wa jiji hilo kama watampa ridhaa ya kuongoza miaka mingine 5 kutatua tatizo la mgao wa maji na kuletewa bili kubwa tofauti na matumizi husika.

https://apps.tsn.go.tz/public/uploads/18c6c5c14d2818717d52db36f2b55bc8.jpg

ALIYEKUWA Mbunge Mteule wa Jimbo la Konde ...

foto
Mwandishi: ALFRED LUKONGE

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi