loader
Dstv Habarileo  Mobile
TPA
Picha

Azam Media mmerudisha thamani ya ngumi

MCHEZO wa ngumi katika nchi zilizoendelea unapewa thamani kubwa na kutazamwa na mamilioni ya watu wengi duniani kutokana na uwekezaji mkubwa uliofanyika kutoka kwa kampuni mbalimbali.

Ukitaja ukanda wa Afrika bado mchezo huo hauna thamani kama soka na wala hakuna mapambano makubwa yaliyowahi kutokea yakajulikana na kutangazwa kama inavyokuwa kwa mataifa mengine ya Ulaya na Marekani kwa miaka ya karibuni.

Kwa upande wa Tanzania, mchezo huo miaka ya hapo nyuma ulikuwa unachukuliwa kama wa watu wahuni kwani ukitizama mashabiki wake walivyo na hata muonekano wa mabondia walikuwa wanaonekana kama 'teja' fulani.

Pengine ni kutokana na namna walivyokuwa wanajiweka na mazingira wanayoishi pia, ni magumu.

Kingine kilichokuwa kinatoa thamani ya mchezo huo ilikuwa ni migogoro isiyoisha, vijembe na fitina zilizokuwa zinaanzia kwa baadhi ya mapromota na viongozi wa mashirikisho ya mchezo huo.

Kwa sasa mambo yamebadilika na unaweza kusema kuwa Serikali ni ya kwanza katika kuufanya mchezo kuwa wenye thamani na kufuatiwa na Azam Media ambao wamejitoa kuurudisha mchezo wenyewe katika kiwango cha juu kwa kudhamini na kuutangaza.

Ukija upande wa serikali baada ya kuwakutanisha wadau wa ngumi na kuunda chombo kimoja kitakachotambua mchezo huo ambacho ni Kamisheni ya ngumi hakika imesaidia kwa asilimia 100.

Chombo hicho kimesaidia kuwafanya mabondia, viongozi na mapromota kuwa na kauli moja. Na hiyo ni kutokana na sheria zilizowekwa ili kuwatambua.

Mchango wa serikali kupitia Baraza la Michezo la Taifa (BMT) kumewarahisishia mabondia hivi leo wanapata udhamini wa Azam Media na wadau wengine wanawaunga mkono.

Kila kukicha kuna wadau wapya wanajitokeza kuandaa mapambano ya kimataifa ya ngumi na hiyo kuonesha ni namna gani mchezo huo umeanza kutambuliwa, kupewa thamani na sasa mashabiki watazidi kuongezeka kadiri siku zinavyokwenda.

Azam Media wana mchango mkubwa waliwahi kuwakutanisha mapromota na mabondia na kuweka ratiba zao vizuri kwa ajili ya mapambano.

Naona miaka ijayo mchezo huo unaweza kuja kuwa na mashabiki wengi kama ilivyo soka na pengine wakaja kujaza uwanja wa Uhuru na kuweka historia nyingine.

Kitendo cha Media hiyo kujihusisha na mchezo huo leo mabondia wanaoandaliwa mapambano makubwa wana uhakika wa kulipwa vizuri na kufanya jambo la maana.

Kuna baadhi ya mabondia wanaheshimika sasa kwa sababu uwekezaji wa Azam unafanya wawe hivyo. Ukikutana na baadhi yao, huwezi kusema ni wahuni kwani namna wanavyovaa ni tofauti na wale tuliokuwa tunawaona miaka kadhaa iliyopita.

Kwa mfano ukimtazama Hassan Mwakinyo, Twaha Kiduku, Nassibu Ramadhan, Abdallah Pazi, Seleman Kidunda na wengine wanaonekana ni watu fulani wanaojiheshimu. Uvaaji wao, namna wanavyoongea na watu huwezi kuwaita ni wavuta bangi kama baadhi ya watu wanavyodhani.

Ukiachilia mbali zile tambo zao ambazo wamekuwa wakizitoa kwa mihemko lakini ni watu wazuri wanaojiheshimu wanapokuwa mtaani, sio wababe kivile kama wanavyotafsiriwa.

Sasa huko nyuma, kuna baadhi ya mabondia walikuwa wanaonesha ubabe hadi mtaani kwao na wengine ilifikia hatua wanahusishwa katika vitendo vya wizi ila siku hizi hayo mambo hayapo tena, thamani yao imerejeshwa na wananufaika kwa wale wanaofanya vizuri.

Ilichofanya Azam kwa kujitoa kuinua mchezo huo, kinatoa mwanga kwa kampuni nyingine kujitokeza kushirikiana nao kwa kuwa, hata wao wenyewe wamekuwa wakiomba hivyo, kwa ajili ya kupeleka mbele mchezo huo.

IFIKE wakati viongozi wa Simba na Yanga wakubali ...

foto
Mwandishi: Grace Mkojera

Post your comments

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi