loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Kaze akunwa na hiki hapa

KOCHA wa Yanga, Cedric Kaze amesema kupata matokeo mazuri ndani ya siku tano ni kitu kigumu ila amefurahi namna wachezaji wake walivyoonesha tumaini japo kidogo la kushika mfumo wake.

Kaze alipata ushindi wake wa kwanza wa bao 1-0 dhidi ya Polisi Tanzania katika mchezo uliofanyika Uwanja wa Uhuru, ikiwa ni siku chache tangu ajiunge nao kuchukua mikoba ya aliyefungashiwa virago, Zlatiko Krmpotic.

Akizungumza na waandishi wa habari juzi baada ya mchezo huo alisema kuna baadhi ya vitu vimemfurahisha kama vile wachezaji kuonesha juhudi kwa kufanya kile alichowaelekeza ingawa kuna muda walikuwa wanasahau.

“Vipindi viwili vilikuwa havifanani jinsi nilivyokuwa nataka, cha kwanza hatukufanya vizuri tulikuwa tunapoteza pasi lakini pia, tulipata nafasi kama tatu za kufunga mabao hatukumalizia vizuri na kipindi cha pili tulijitahidi kiasi, ila najua watazoea taratibu,” alisema.

Alisema kilichomfurahisha zaidi ni vile wachezaji wake walivyojitahidi kucheza mpira mwanzo mpaka mwisho na kupata pointi tatu muhimu.

Kaze alisema matarajio yake ilikuwa ni ushindi, alitamani kuona wachezaji wakitembea na mpira na kumiliki kitendo ambacho wamejitahidi, lakini sio kama alivyotaka akisema ni suala la muda tu watazoea taratibu.

Alisema wanachoangalia kwa sasa ni mchezo ulioko mbele yao dhidi ya KMC kujipanga kwenda Mwanza kwa ajili ya kupigania pointi tatu.

Kwa upande wa kocha wa Polisi Tanzania, Malale Hamsini alisema wanajilaumu wenyewe kwa kupoteza mchezo huo kwani walikuwa wana nafasi ya kumaliza mchezo mapema kama wangetumia vizuri nafasi walizopata.

Alisema vijana wake walijituma kwa kucheza mchezo mzuri kilichowaangusha ni kushindwa kutumia vizuri nafasi walizopata.

 

TIMU ya soka ya taifa, Taifa ...

foto
Mwandishi: Grace Mkojera

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi