loader
Dstv Habarileo  Mobile
TPA
Picha

Prisons wakana kuikamia Simba

NAHODHA wa kikosi cha Tanzania Prisons, Benjamin Asukile amesema hawakuwa wameikamia Simba katika mchezo wa juzi bali waliwaheshimu na kuingia kwa kujiamini ndio maana walipata ushindi.

Prisons ilishinda bao 1-0 dhidi ya Simba katika mchezo wa Ligi Kuu uliochezwa juzi, Uwanja wa Nelson Mandela mjini Sumbawanga.

Akizungumza baada ya mchezo huo, Asukile alisema walijua uwezo wa wapinzani wao ni mkubwa ila wao walijipanga na kucheza kwa umoja uliowasaidia kupata pointi tatu.

“Tulijipanga kucheza kwa kujiamini na kuwaheshimu wapinzani wetu tukijua na uwezo wao. Kocha alikuwa na mipango yake ambayo imetuwezesha kushinda,”alisema.

Alisema ushindi walioupata haimaanishi wao ni bora kuliko Simba isipokuwa wao walikuwa bora katika mchezo huo walioibuka na ushindi.

Ushindi huo uliipandisha Prisons kutoka nafasi ya 14 hadi ya nane ikifikisha pointi tisa, huku Simba ikishuka kutoka nafasi ya pili hadi ya tatu kwa pointi zake 13.

Kwa upande wa nahodha wa Simba, Mohamed Hussein ‘Tshabalala’  alisema wenzao wamepata nafasi wameitumia ila wao walishindwa kutumia na ndivyo mchezo ulivyo.

Alisema tayari wamepoteza mchezo huo wanarudi kujipanga kwa mchezo ujao kuhakikisha wanarekebisha makosa na kufanya vizuri.

 

IFIKE wakati viongozi wa Simba na Yanga wakubali ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu

Post your comments

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi