loader
Dstv Habarileo  Mobile
TPA
Picha

Ihefu, Mbeya City viwanjani leo

TIMU ya soka ya Ihefu na Mbeya City leo zitashuka dimbani katika viwanja viwili tofauti zikiwa na makocha wengine kwa ajili ya kusaka ushindi katika mchezo wa Ligi Kuu soka Tanzania Bara.

Ihefu chini ya kocha mpya, Zuberi Katwila tayari imetoka kupoteza mchezo uliopita dhidi ya Azam FC mabao 2-0 na leo ina kibarua kingine cha kuwakaribisha Namungo kwenye Uwanja wa Sokoine, Mbeya.

Mchezo huo ni mgumu hasa kwa wenyeji walioko nafasi za chini kwa kuwa timu itakuwa na presha kutokana na mwenendo wake mbaya uliopita lakini huenda kocha huyo akaja na mbinu mpya zitakazomwezesha kupata matokeo mazuri baada ya kuona mchezo uliopita.

Aidha, Namungo nayo imekuwa ikisuasua kutafuta matokeo mazuri na kurudi katika nafasi za juu.

Mwenendo wake awali haukuwa mzuri ila mchezo uliopita walipoteza dhidi ya Mtibwa bao 1-0 watakuwa kwenye presha ya kutafuta matokeo mazuri.

Mechi nyingine itakuwa ni Coastal Union dhidi ya Gwambina kwenye uwanja wa Mkwakwani, Tanga.

Coastal wakipoteza mchezo huo watazidi kushuka kwani nafasi waliyopo wanahitaji kushinda ili kupanda juu. Mchezo uliopita walishinda mabao 3-0 dhidi ya Biashara United.

Kwa upande wa Gwambina imetoka kupata sare mchezo uliopita dhidi ya Polisi Tanzania, wanahitaji ushindi kuendelea kupanda nafasi za juu.

Kagera Sugar itachuana na Mbeya City katika uwanja wa Kaitaba, mchezo ambao ni mgumu pande zote mbili.

Mbeya City inanolewa na Kocha Msaidizi, Mathias Wandiba baada ya kumtimua Kocha Mkuu, Amri Said aliyekuwa na mwenendo mbaya wa matokeo tangu kuanza kwa msimu huenda mambo yakawa mazuri.

Kagera haikuwa na matokeo mazuri katika mechi tatu zilizopita, baada ya kufungwa miwili na mwisho waliocheza dhidi ya Dodoma Jiji wametoka kupata suluhu hivyo, ni lazima wapambane kuondoka hatarini.

FAINALI ya shindano la Safari Lager Nyama Choma ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu

Post your comments

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi