loader
Dstv Habarileo  Mobile
TPA
Picha

Utafiti wabaini asilimia 30 mafuta, gesi Z’bar

RAIS wa Zanzibar, Dk Ali Mohamed Shein amewasilisha taarifa za awali za matokeo ya utafiti wa mafuta na gesi ambayo inaonesha kuwepo kwa kiwango kikubwa cha rasilimali hiyo kwa asilimia 30 katika visima vilivyopo Unguja na Pemba.

Akizungumza na waandishi wa habari Ikulu, Dk Shein alisema kiwango cha asilimia 30 ni sawa na ujazo wa trilioni 3.8 ambapo kinaweza kuongezeka zaidi kwa kufanya utafiti zaidi wa kina na kufikia asilimia 45.

“Ndugu waandishi wa habari na wananchi kwa ujumla napenda kutoa taarifa za awali za utafiti wa nishati ya mafuta na gesi asilia unaonesha kuwepo kwa viashiria vya rasilimali hiyo kwa asilimia 30...utafiti zaidi utafanyika ambao yapo matumaini ya kupatikana kwa nishati hiyo kwa asilimia 45,” alisema.

Dk Shein alisema utafiti huo ambao umefanywa na kampuni ya Rak Gas kutoka nchini Rasilkhema ulifanywa katika njia tatu ikiwemo mtetemo, nchi  kavu pamoja na angani na sehemu yenye kina kirefu cha maji Unguja na Pemba.

Hata hivyo, aliwatanabaisha wananchi kuwa kazi za kuanza kuchimba rasilimali ya nishati ya mafuta na gesi inaweza kuanza baada ya miaka sita hadi minane baada ya kukamilika kwa uchunguzi.

Dk Shein alichukuwa nafasi hiyo kuipongeza serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania chini ya uongozi wa Rais mstaafu Dk Jakaya Kikwete kwa kuchukua uamuzi wa kuliondoa suala hilo katika mambo ya orodha ya Muungano.

Alisema hatua hiyo ndiyo imetoa nafasi kwa Zanzibar kuanza kufanya utafiti wa mafuta na gesi katika maeneo ya Unguja na Pemba pamoja na kufungua shirika litakalosimamia kazi za nishati hiyo.

“Napenda kuwajulisha wananchi kwamba suala la mafuta na gesi sasa limeondolewa rasmi katika mambo yaliopo katika orodha ya mambo ya Muungano...ndiyo maana Zanzibar sasa ruhusa kufanya kazi za utafiti pamoja na kuchimba mafuta,” alisema.

Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania lilitunga Sheria namba 21 ya mwaka 2015 na kupitishwa Julai 2 mwaka 2015 ambayo iliondoa suala la mafuta na gesi miongoni mwa mambo yaliopo katika orodha ya Muungano.

Aidha, Dk Shein alisema Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ) imejipanga kukabiliana na hatua mbalimbali za uharibifu wa mazingira wakati rasilimali ya mafuta na gesi itakapoanza kuchimbwa.

Alisema tayari uchambuzi wa kitaalamu wa kimazingira umefanywa kwa kufanya utafiti wa nchi mbalimbali ambazo zilichimba mafuta na kuzalisha nishati hiyo.

“Suala la uhifadhi wa mazingira tumelifanyia kazi na kupewa kipaumbele cha kwanza...tumejifunza kwa nchi za wenzetu kuhusu hatari za athari ya uharibifu wa mazingira na tupo tayari kukabiliana nazo,” alisema.

Kwa mfano alisema katika utafutaji wa mafuta kwa nia ya anga, imebainika kuwepo kwa maeneo matatu yenye uwezo wa kuwepo kwa miamba inayoweza kuhifadhi rasilimali ya mafuta na gesi ikiwemo kisiwa cha Makoongwe Pemba na kusini mwa kisiwa cha Tumbatu kiliopo Unguja.

MSANII wa Bongo fl eva , Zuwena Mohammed ...

foto
Mwandishi: Khatib Suleiman, Zanzibar

Post your comments

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi