loader
Dstv Habarileo  Mobile
TPA
Picha

Serikali kushirikiana na sekta binafsi kukuza ujuzi

WIZARA  ya Elimu, Sayansi na Teknolojia  itaendelea  kushirikiana na sekta binafsi katika kuhakikisha inakuza ujuzi na stadi za kazi ili kulisaidia taifa liwe na nguvu kazi ya kutosha inayoweza kuajirika kwenye soko la ajira.

Mkurugenzi wa Elimu, Sayansi na Teknolojia wa Wizara hiyo, Dk Noel Mbonde alisema hayo juzi mjini hapa wakati wa kikao cha wakurugenzi wa sera na mipango kuhusu uanzishwaji wa Baraza la Taifa la Ujuzi la Kisekta nchini.

Dk Mbonde alisema mpango huo unahusisha sekta sita za kipaumbele zilizoainishwa katika mpango mkakati ambazo ni sekta ya kilimo, nishati, ujenzi, utalii, uchukuzi na usafirishaji.

Alisema kuwepo kwa ushirikiano kutoka sekta binafsi ni jambo zuri katika kuhakikisha kuwa masuala yanayopangwa kutekelezwa kwenye mabaraza ya ujuzi ya kisekta yanafanikiwa kwa kiwango kikubwa.

"Serikali inatambua na inakubali kwamba sekta binafsi ndiyo injini ya ukuaji wa uchumi nchini,” alisema Dk Mbonde.

Akaongeza: "Serikali itafanya kila liwezekanalo kuiwezesha sekta binafsi katika kukuza ujuzi ili kufanikiwa kuwa na Taifa lenye nguvu kazi yenye ujuzi na stadi stahiki unaohitajika kwenye soko la ajira."

Naye  Mkurugenzi Mtendaji wa Chama cha Waajiri Tanzania (ATE), Dk Aggrey Mlimuka alisema kuwa njia zinazotumika kuhakikisha vijana wanapata ujuzi ni pamoja na masomo kwa vitendo, kuwapa nafasi katika maeneo mbalimbali ya kazi  na mafunzo tarajali.

"Kijana atafanya mafunzo si chini ya miezi sita na wanaopitia katika njia hizi tatu huwa wanapata kazi kwa urahisi kwa waajiri wao," alisema.

Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi (NEEC), Beng'i Issa, alisema sekta binafsi zina mchango mkubwa katika kukuza uchumi wa Taifa.

"Ujuzi unaweza kukuza uchumi wa nchi na vijana wetu wana elimu ya kusomea ambayo haiwavutii  sana waajiri kutokana na kukosa elimu ya ujuzi," alisema Issa.

Awali, Mshauri Mwelekezi wa Mabaraza ya Ujuzi ya Kisekta  nchini, Nicholas Mbwanji alisema baraza kwa sasa limejikita zaidi kuhusu namna ya kuwa na mfumo utakaotumika  kwa ajili ya kutoa mafunzo  na namna ya kutatua changmoto mbalimbali.

Mbwanji alisema kuna vigezo vinne ambavyo vinapimwa katika uendeshaji wa masuala ya kukuza ujuzi ambayo ni  sheria, utawala, fedha, ushirikiano baina ya tasisi moja na nyingine.

MSANII wa Bongo fl eva , Zuwena Mohammed ...

foto
Mwandishi: John Nditi, Morogoro

Post your comments

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi