loader
Dstv Habarileo  Mobile
TPA
Picha

Wahimiziwa kuwahi vituo vya kupigia kura

MGOMBEA ubunge kupitia Chama Cha Mapinduzi(CCM) katika jimbo la Ilemela, Dk Angelina Mabula amewasisitiza wakazi wa Ilemela kuhakikisha siku ya uchaguzi Oktoba 28 mwaka huu wanawahi katika vituo vya kupigia kura na kaisha kurejea majumbani kwao.

Rai hiyo alitoa wakati wa mkutano wake wa mwisho katika kata ya Kitangiri kwenye viwanja vya Minazi Mitatu. Dk Mabula aliwaomba wakazi wa Ilemela kuhakikisha wanaendelea kukichagua Chama Cha Mapinduzi(CCM) na wagombea wote wanaotokana na chama hicho.

Dk Mabula aliahidi pia kuboresha miundo mbinu ya soko ya Kitangiri. Dk Mabula alisema  tayari Serikali ya CCM imetenga milioni 300 kwajili ya ujenzi wa mwalo wa Mihama  uliopo katika kata hiyo.

Aliahidi kuhakikisha atajenga barabara za Jiwe kuu kuelekea Mihama katika kiwango cha lami na tayari milioni 67/- zimetengwa kwajili ya ujenzi huo. Katika sekta ya Elimu,Dk Mabula alisema katika wilaya ya Ilemela wamefanikiwa kujenga madarasa 69 kwa shule za msingi na madarasa 54 katika shule za sekondari za wilaya yao.

Alisema tayari wametenga milioni 39 kwajili ya kujenga  madarasa matatu katika shule ya sekondari ya Mwinuko na milioni 30 kwajili ya kujenga maabara katika shule hiyo. Alisema wametenga pia milioni 10 kwajili ya kujenga nyumba ya katika shule ya sekondari Mihama.

MBUNGE  wa Mkuranga Abdallah Ulega anatarajiwa kufanya ziara ...

foto
Mwandishi: Na Mwandishi Wetu

Post your comments

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi