loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Watanzania wasikubali kubinafsisha mashirika makubwa-JPM

Rais wa Tanzania Dk. John Magufuli amesema kuwa watanzania wasikubali tena kubinafsisha mashirika makubwa bila sababu za msingi.

Rais Dk. Magufuli amesema hayo leo jijini Arusha katika uzinduzi wa safari za Treni kutoka Dar es Salaam,Tanga, Moshi hadi Arusha.

Amesema kuwa nchi zilizoendelea duniani mashirika makubwa kama ya Reli na Ndege hubaki mikononi mwa serikali kama njia mojawapo ya  kupunguza gharama za huduma kwa wananchi wa hali ya chini.   

Aidha, Dk Magufuli alimpongeza Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Reli Tanzania (TRC) Masanja Kadogosa kwa imani yake kwa  mafundi wazawa kwenye ukarabati wa mabehewa 347 na vichwa 11 jambo lililoongeza ufanisi wa kiutendaji kwenye shirika hilo.

“Vichwa vya watanzania vina akili mno, ila tatizo letu atuaminiani kupitia mfano huu waliouonyesha TRC inatupasa kuanza kuaminiana kuwa tunaweza kwenye ufanikishaji wa mambo mbalimbali sisi wenyewe” amesema Rais Dk Magufuli.

 

 

 

 

NAIBU Waziri wa Mifugo na Uvuvi, ...

foto
Mwandishi: Alfred Lukonge

1 Comments

  • avatar
    Elias pusindawa
    24/10/2020

    Ili mafanikio yoyote yatokee ni lazima maamuzi magumu yafanyike hivyo kongole kwa rais magufuli kwa haya anayoyafanya

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi