loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Wakalimani watakiwa kupunguza gharama

WAKALIMANI wa lugha ya alama mkoani Pwani, wametakiwa kupunguza gharama za kutafsiri ili vyama na vyombo vya habari, viweze kumudu kuwatumia wakati wa kampeni za uchaguzi mkuu zinazoendelea.

Akizungumza na HabariLeo mjini Kibaha, Mlezi wa Umoja wa Watu Wenye Ulemavu (UWP) Mkoa wa Pwani Robert Bundala alisema kuwa viziwi wengi hawawezi kupata taarifa kutokana na kutokuwa na wakalimani wa lugha ya alama kwenye mikutano ya hadhara ya kampeni au kupitia luninga.

Bundala alisema kuwa wakati huu wa kampeni, kila mtu ana haki ya kupata taarifa za wagombea wakati wakinadi sera zao ili waweze kuchagua viongozi bora.

Lakini alisema kutokana na gharama kubwa za wakalimani, vyama na vyombo vya habari vinashindwa kuwatumia wakati wa mikutano ya kampeni.

“Baadhi ya watu wenye ulemavu mwingine kidogo wana uwezo wa kusikia kinachozungumzwa na wagombea lakini viziwi wao hawana uwezo wa kusikia kinachozungumzwa. Ili wakati wa upigaji kura wachague kiongozi mwenye sera nzuri, wakalimani hao wapunguze gharama ili huduma yao itumike," alisema Bundala.

Alisema kuwa hiyo ni huduma na siyo biashara, hivyo kuna haja ya wakalimani hao kupunguza gharama za ukalimani ili vyama vya siasa viwatumie kwenye mikutano ya kampeni na vyombo vya habari.

Akizungumzia watu wenye ulemavu kuwania nafasi za uongozi, alisema baadhi ya vyama hasa vile vidogo vimeweka baadhi ya wagombea wenye ulemavu. Aliongeza kuwa baadhi ya vyama hasa vile vikubwa, vimetenga nafasi za watu wenye ulemavu lakini siyo nafasi za moja kwa moja.

Aliishukuru Tume ya Taifa ya Uchaguzi kwa kuweka mazingira mazuri kwa watu wenye ulemavu. Aliiomba tume hiyo kuwapa nafasi watu wenye ulemavu kupiga kura, badala ya kukaa kwenye foleni.

NAIBU Waziri wa Mifugo na Uvuvi, ...

foto
Mwandishi: John Gagarini, Kibaha

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi