loader
Dstv Habarileo  Mobile
TPA
Picha

‘Wazazi shirikianeni na serikali sekta ya elimu

WAZAZI nchini wameaswa kuisaidia serikali kutatua baadhi ya changamoto zinazoikabili sekta ya elimu na kuunga mkono jitahada za ujezi wa madarasa pamoja na ununuzi wa vifaa vya kufundishia shuleni.

Hatua hiyo inaelezwa itaongeza kasi ya upatikanaji wa elimu bora nchini. Wito huo ulitolewa na Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya uhandisi wa umeme na mitambo viwandani na migodini ya Magare ya jijini Mwanza, Mabula Magangila wakati wa mahafali ya kidato cha nne ya Shule ya Sekondari Isagehe, wilayani Kahama, mkoa wa Shinyanga.

Magangila ambaye pamoja na kuwa mgeni rasmi katika mahafali hayo, pia aliwahi kusoma katika shule hiyo.

Alisema katika kipindi hiki ambacho serikali inapambana kutatua changamoto zinazoikabili sekta ya elimu nchini ipo haja kwa jamii kuiunga mkono kwa kujitolea katika kutatua changamoto zinazozorotesha ustawi wa sekta hiyo muhimu.

“Ni vema changamoto zinazoikabili sekta ya elimu tuzitatue kwa pamoja. Ongezeko la wanafunzi limesababisha uhaba wa madarasa, walimu na vifaa vya kufundishia na hatuwezi kusubiri serikali peke yake itatue changamoto hizi.

Ipo haja kwa wazazi na wadau kama sisi wafanyabiashara tunaotoa huduma katika wilaya hii kujitokeza ili tuongeze nguvu,’’ alisema.

Katika kuiunga mkono serikali katika sekta hiyo, Magangila alitangaza uamuzi wake wa kuajiri walimu sita wa ziada watakaolipwa mshahara na kampuni yake ya Magare ili waweze kusaidiana na walimu wa shule hiyo kufundisha masomo ya sayansi na biashara kutatua changamoto ya uhaba wa walimu wa masomo hayo shuleni hapo.

“Binafsi nimefika hapa nilipo kwa kusaidiwa sana na walimu wa ziada kwa kuwa walimu walikuwa hawatoshi. Naomba mkuu wa shule atusaidie kutafuta walimu wa ziada wenye sifa za kufundisha masomo ya sayansi na biashara.

Kampuni ya Magare tupo tayari kuwalipa mishahara yao ili waongeze nguvu wakati tunasubiri serikali ituletee walimu wa kutosha,” alisema.

Alisema kampuni hiyo itamalizia ujenzi wa maboma ya vyumba vya madarasa matatu katika shule hiyo pamoja na kusaidia ununuzi wa mashine ya kisasa ya kudurufu, printa na kompyuta kwa ajili ya kusaidia shughuli za maandalizi ya mitahani ya wanafunzi hao, huku pia akitoa mchango wa Sh milioni moja kwa ajili ya kufikisha mtandao wa maji safi na salama katika shule hiyo.

Aliwashakuru wadau mbalimbali ikiwamo migodi ya dhahabu ya Bulyanhulu na Buzwagi ambao ni wateja wa Magare kwa namna wanavyosaidia maendeleo ya elimu katika wilaya ya Kahama ikiwamo shule hiyo ambapo mgodi wa Buzwagi unasaidia ujenzi wa bweni la wanafunzi.

Mkuu wa shule hiyo, Adolf Kabyemela na Mwenyekiti wa Bodi ya shule hiyo, Castor David walimshukuru Magangila na kampuni yake, huku wakiahidi kuongeza kiwango cha ufaulu wa wanafunzi wa kidato cha nne ambao licha ya wengi wao kufanya vizuri kidato cha pili lakini wamekuwa wakishindwa kufanya vizuri kidato nne

MBUNGE  wa Mkuranga Abdallah Ulega anatarajiwa kufanya ziara ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu, Shinyanga

Post your comments

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi