loader
Dstv Habarileo  Mobile
TPA
Picha

CUF yataka udiwani Chololo kuondoa changamoto sugu

KATIBU wa Chama cha Wananchi (CUF) Wilaya ya Kondoa mkoani Dodoma, Juma Athumani amesema kama wananchi watamchagua diwani kutoka chama hicho atawaondolea wananchi hao tatizo la kutembea umbali wa kilomta 11 kufuata huduma ya mama na mtoto inayopatikana katika kata ya Chololo iliyopo Kondoa Vijijini.

Athumani alisema hayo alipokuwa akimnadi mgombea wa udiwani kwenye Kata ya Chang’ombe iliyopo wilaya ya Kondoa mjini, Hamidu Kadogoo katika mkutano wa kampeni uliofanyika viwanja vya Chang’ombe.

Aliwataka wananchi wa kata hiyo kutofanya makosa kwa kuchagua viongozi ambao hawana sera za kuwaletea maendeleo, ambayo hivi sasa yanahitaji kwa watanzania wote bila kujali itikadi ya kabila na dini.

“Kichagueni chama cha CUF ili kikawaondolee changamoto ambazo zimekuwa sugu kwenye maeneo mnayoishi ikiwemo maji, umeme, zahanati, elimu, ufugaji na upande wa kilimo pia,”alisema.

Naye mgombea udiwani wa kata hiyo kupitia chama hicho, Hamidu Mkopi aliwaomba wakazi wa kata hiyo ya Chang’ombe kumchagua ili aweze kufanikisha kutatua changamoto walizokuwanazo ikiwemo la maji.

Alisema kwenye kata hiyo changamoto kubwa iliyopo ni upatikanaji wa maji salama ya uhakika ambayo hivi sasa upatikana kwenye visima vya kienyeji na korogoni ambako hata hivyo wanyama pia wanayatumia.

MBUNGE  wa Mkuranga Abdallah Ulega anatarajiwa kufanya ziara ...

foto
Mwandishi: Sifa Lubasi, Kondoa

Post your comments

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi