loader
Bilioni 5/- zanunua dawa Manispaa Lindi

Bilioni 5/- zanunua dawa Manispaa Lindi

MJUMBE wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Kassim Majaliwa amesema katika miaka mitano, Serikali imetumia shilingi bilioni 5.26 kununua dawa kwenye Manispaa ya Lindi.

Aliyasema hayo wakati akizungumza na wakazi wa mji wa Lindi na vitongoji vyake kwenye mkutano wa kampeni katika uwanja wa Ilulu mjini Lindi.

“Serikali imetoa shilingi bilioni 5.26 ambapo kati ya hizo, shilingi bilioni 4 zilikuwa za Hospitali ya Rufaa ya Sokoine na shilingi bilioni 1.26 zilitolewa kwa Halmashauri ya Manispaa ya Lindi kwa ajili ya ununuzi wa dawa, vifaa tiba na vitendanishi.

Fedha za ununuzi wa dawa kwa mwezi, ni wastani wa shilingi milioni 21,” alisema Majaliwa. Kuhusu maboresho kwenye sekta ya afya haji wa sekta ya afya, alisema katika Manispaa ya Lindi, kuna magari matano ya kubeba wagonjwa kwa ajili ya vituo vya afya Mjini, Mnazimmoja, Kitomanga, Milola na Rutamba.

Majaliwa alikwenda Lindi kumuombea kura mgombea urais wa Tanzania kupitia CCM John Magufuli. Alitumia fursa hiyo kuwaombea kura mgombea ubunge jimbo la Lindi, Hamida Abdallah na wagombea udiwani kwenye kata 20 za jimbo hilo.

Kuhusu sekta ya maji, alisema sh. bilioni 50 zimetolewa kwa ajili ya miradi mikubwa ya maji ukiwemo ujenzi wa skimu ya pampu Mtutu, skimu ya pampu Cheleweni, Narunyu, Tandangongoro na Muungano na kwamba zimesaidia kuongeza upatikanaji maji kwenye mji wa Lindi.

“Fedha hizo zimetumika pia kwa ajili ya mradi wa maji safi na usafi wa mazingira Lindi Mjini na kwenye mradi wa maji Ng’apa kijijini na usambazaji mtandao wa mabomba,” alisema.

Alisema shilingi bilioni 1.26 zilitolewa kwa ajili ya miradi mingine ya maji ikiwa ni pamoja na kuchimba visima virefu Jangwani, Nanyanje, Kitumbikwela, Nachingwea, Kitunda, Likotwa, Mtange, Tulieni, Mitumbati, Mayani na Ngongo-Nanenane

foto
Mwandishi: Mwandishi Maalumu, Lindi

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi