loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Zidane atetea penati dhidi ya Barca

ZINEDINE Zidane ametetea maamuzi ya penati yaliyoisaidia timu yake Real Madrid kushinda mabao 3-1 kwenye mechi ya El Clasico dhidi ya Barcelona Camp Nou mwishoni mwa wiki iliyopita.

Mechi hiyo ya La Liga ilikuwa sawa baada ya mabao ya kipindi cha kwanza kutoka kwa Federico Valverde na Ansu Fati pale Sergio Ramos na Clement Lenglet kuumizana ndani ya 18.

Mwamuzi Juan Martinez Munuera aliona jezi ya nahodha wa Real Madrid ikivutwa na beki wa Barca baada ya kutizama VAR na Ramos akafunga mkwaju wa penati kabla Luka Modric hajaiwezesha timu yake kupata pointi tatu baadae.

“Kulikuwa na mwamuzi. Alitizama na kutoa penalti,” Zidane alisema kwenye mkutano na waandishi wa habari baada ya mechi hiyo. “Huwa sizungumzii kuhusu waamuzi, ni kazi ngumu na sitaki nianze leo (juzi) alitizama tena na kuona ilikuwa penati, tulistahili kushinda na imeisha kwa 3-1, tungeweza kufunga zaidi.”

Zidane aliingia kwenye mechi hiyo akiwa mwenye shinikizo baada ya Madrid kupoteza mechi mbili ndani ya wiki moja, akifungwa na Cadiz kwenye La Liga na Shakhtar Donetsk kwenye Ligi ya Mabingwa.

“Tulihitaji kurejea kwenye kujiamini na mechi hii ilikuwa nzuri kwa jambo hilo,” alisema.

“Sijui kama ni watu hawaitendei haki timu au mimi, lakini timu hii ina utaratibu wake, hatupo hapa kunyamazisha watu. Kazi yetu ni kuamini tunachokifanya, kuwa pamoja na leo (juzi) ndicho tulichofanya,” alisema.

Nahodha Ramos alikuwa kwenye hatihati ya kucheza mechi hiyo kutokana na kuwa majeruhi, akikosa mechi mbili ziliozpita kutokana na kusumbuliwa na goti lakini alirejea kikosini na kufunga bao lake la 25 la Penalti.

“Wote Lenglet na mimi tulikuwa kwenye hali mbaya. Ilikuwa penati bila shaka alinichezea vibaya, mwamuzi aliona hakunitendea haki.”

“Ilikuwa ni wiki ya kujisahihisha makosa yetu, lakini la zaidi ni Clasico inaleta hamasa zaidi, tusingeweza kukaa kwenye mwenendo mbaya wa kushindwa mechi mbili mfululizo, tulipaswa kufanya vizuri bila kujali malalamiko ya watu,” alisema Ramos.

Matokeo hayo yameifanya Real Madrid kuwa mbele kwa pointi sita dhidi ya Barca kwenye msimamo wa La Liga, ikiwa imecheza mechi moja zaidi.

Wana kibarua cha kucheza mechi ya Ligi ya Mabingwa wiki hii, wakijipanga kukaa sawa baada ya kufungwa mabao 3-2 na Shakhtar, sasa wakitakiwa kurekebisha makosa kwa Donetsk ugenini Borussia Monchengladbach kesho.

MANCHESTER United leo itaikaribisha Liverpool katika ...

foto
Mwandishi: BARCELONA, Hispania

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi