loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Ubahili waiponza Manchester United

GAZETI la the Sun la limeibua siri nzito kuwa klabu ya Manchester United iliponzwa na ubahili na kushindwa kukamilisha kumsajili Dayot Upamecano miaka mitano iliyopita.

Kwa sasa Upamecano ni mmoja kati wa mabeki ghali duniani na kuwindwa na klabu kubwa kutokana na anachokifanya uwanjani.

Beki huyo raia wa Ufaransa anayekipiga kwenye klabu ya RB Leipzig alisajiliwa kwa pauni milioni tisa mwaka 2017 na sasa thamani yake imefikia pauni milioni 55.

Imeelezwa kuwa, Man U ambayo inasumbuliwa na safu ya ulinzi iliona ubahili kutoa pauni 200,000 mwaka 2015 wakati beki huyo alipokuwa akiitumikia Valenciennes.

Kama Man U wangempata Upamecano ingekuwa ni moja kati ya klabu yenye ukuta mgumu, lakini ilishindwa kumpata baada ya kulazimisha itoe pauni 500,000 huku klabu yake ikihitaji 700,000.

Beki huyo alifika kwenye viunga vya Manchester lakini mabosi walikuwa hawamuamini kutokana na umri wake mdogo kipindi hicho ambapo alikuwa na umri wa miaka 16 licha ya kuitwa kwenye kikosi cha timu ya taifa chini ya umri wa miaka 17.

Ubahili wa Man U umeigharimu baada ya kumsajili Harry Maguire kwa usajili wa rekodi kwa mabeki pauni miliomi 80 mwaka 2019, kisha zikawatoka pauni milioni 31 kumsajili Victor Lindelof na pauni milioni 27 kwa Luke Shaw lakini safu yao inaonekana haijatulia.

Hivi karibuni kutokana na ubovu wa safu yao ya ulinzi klabu hiyo ilijikuta ikipokea kipigo cha mabao 6-1 kutoka kwa Tottenham

ENGLAND jana ilianza vizuri kampeni za ...

foto
Mwandishi: MANCHESTER, England

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi