loader
Dstv Habarileo  Mobile
TPA
Picha

Polisi waagizwa kulinda amani kwa gharama yoyote

MKUU wa Jeshi la Polisi Tanzania (IGP), Simon Sirro amesema nchi iko shwari na pia jeshi hilo lipo tayari kulinda amani wakati wa Uchaguzi Mkuu.

IGP Sirro alisema mjini hapa kuwa, wanaojidanganya kutaka kuleta vurugu katika kipindi hicho watadhibitiwa na kuchukuliwa hatua kali kwa mujibu wa sheria. IGP Sirro alisema hayo jana baada ya kuzungumza na zaidi ya askari 710 wa Mkoa wa Arusha wakiwemo Polisi, Uhamiaji, Magereza na askari mgambo.

Katika mkutano huo aliwaagiza askari hao wailinde amani kwa gharama yoyote kwa maslahi ya nchi. “Wanaopanga kuleta vurugu na uvunjifu wa amani katika kipindi cha uchaguzi waache mara moja kwani wanajidanganya Polisi na majeshi yote yako imara kuilinda amani kwa gharama yoyote’’alisema IGP Sirro

Alisema kuna taarifa za kiintelijensia kwamba kuna vikundi vimejipanga kufanya vurugu wakati wa uchaguzi na kabla ya kutangazwa matokeo ya urais, ubunge na udiwani.

“Tutawashughulikia kabla, najua Arusha miaka ya nyuma kulitokea fujo, kwa hiyo ni mahala ambako tumepanga kuweka askari wa kutosha.

Askari wa kiraia, askari wa oparesheni, askari wa upelelezi wote timamu kuhakisha kwamba Arusha inakuwa shwari” alisema IGP Sirro.

Alisema, Polisi wapo tayari kupambana na vikundi hivyo kwa njia yoyote. “Nchi iko shwari na itakuwa shwari hadi kipindi chote cha uchaguzi na hadi utangazaji wa matokeo ya ngazi zote kwani polisi na majeshi yote yako kazini kuhakikisha nchi inakuwa salama muda wote’’alisema IGP Sirro.

Alisema Polisi wapo ili kulinda raia na mali zao hivyo hawawezi kuona nchi inaingia kwenye machafuko kwa sababu ya watu wachache kwa maslahi yao binafsi.

MKURUGENZI Mkuu wa Ofisi ya Takwimu ya Taifa (NBS), ...

foto
Mwandishi: John Mhala, Arusha

Post your comments

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi