loader
Dstv Habarileo  Mobile
TPA
Picha

Shibuda ataka wagombea wajiandae kisaikolojia

MWENYEKITI wa Baraza la Vyama vya Siasa Tanzania, John Shibuda amewasihi wagombea wa urais wa Tanzania na Zanzibar, ubunge na udiwani kujiandaa kisaikolojia na wawe tayari kupokea matokeo ya kushinda au kushindwa.

Shibuda ambaye pia ni mgombea nafasi ya urais kupitia Chama Cha ADA-TADEA, alisema jana kuwa amefanya kampeni kidijitali na kuwafikia wapigakura kwa njia ya mtandao.

Aliyasema hayo jana jijini Dodoma wakati akizungumza na waandishi wa habari. “Niwasihi kila mgombea ajiandae kisaikolojia na kwa moyo mkunjufu awe tayari kupokea matokeo ya ushindi au ya kushindwa.

Kila mgombea akubali somo la kuwa asiyekubali kushindwa siyo mshindani, na kuvunjika kwa jembe siyo mwisho wa uhunzi. Pia asiyekubali subra za kuongozwa na mwenzake hana sifa za kuitwa kiongozi wa jamii,”alisema Shibuda.

Alisema kama Tanzania ingekuwa inachagua kapteni wa timu ya mpira ana uhakika kura nyingi zingekwenda kwa John Magufuli.

Alitumia fursa hiyo kuwakumbusha wagombea na mashabiki wa vyama vya saisa kuwa ushindi hautokani na taswira ya hadhara zilivyokuwa katika mikutano ya kampeni.

“Maajabu ya siku ya kupiga kura hutoa somo ambalo lina jibu kuwa kuwepo umati wa watu wengi katika mikutano siyo nyenzo ya matokeo ya tarakimu halisi za namna za takwimu za hesabu za idadi ya wapigakura za NDIO na za kutoa ushindi.”

Shibuda alisema wapigakura wana vigezo vyao vya kutoa kura za ndio za kutoa ushindi ambavyo ni chema hujiuza, kibaya chajitembeza.

“Kura nyingi zinaenda kwa yule aliyegusa hisia za umma na anayekonga mioyo ya umma kwa vielelezo vya kauli za kutoa ujumbe wa kuwa ana matendo ya sifa za hisia za uzalendo”alisema na kuongeza; “Wapigakura hupenda mgombea wa sifa za mfano wa uzalendo wa kuneemesha nchi kupitia maliasilia na rasilimali za Taifa ni mtaji wa kuwezesha usalama wa azma ya kutimiswa kilio uhuru, kujitegemea.”

Alihimiza wananchi watumie haki yao ya kupigakura keshokutwa na waitumie kwa manufaa mapana ya taifa, kwa leo na siku zijazo.

MKURUGENZI Mkuu wa Ofisi ya Takwimu ya Taifa (NBS), ...

foto
Mwandishi: Anastazia Anyimike, Dodoma

Post your comments

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi