loader
Majaliwa asema mataifa nje yanamtamani JPM

Majaliwa asema mataifa nje yanamtamani JPM

MJUMBE wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Chama cha Mapinduzi (CCM), Kassim Majaliwa amesema, kutokana na uwezo wa Rais John Magufuli kuna nchi zinatamani akawe kiongozi huko kwao hata kwa miezi sita.

Majaliwa alisema jana mjini Liwale kuwa, Serikali ya Awamu ya tano imefanya mambo mengi makubwa na ndio maana Magufuli anatajwa kuwa Rais mwenye mafanikio zaidi Afrika.

Aliomba wananchi wamchague Magufuli aendelee kuiongoza Tanzania kwa kuwa ana uwezo wa kuunda serikali imara na kuisimamia itumikie Watanzania na hakuna mgombea mwenye sifa za kuleta maendeleo kama yeye (Magufuli).

“Watanzania tunataka tumchague Rais tunayemjua”alisema Majaliwa na kuongeza kuwa, kazi ya urais si ya majaribio hivyo wananchi wanapaswa kumchagua mgombea kwa ajili ya maendeleo na si kwa ushabiki.

Kwa mujibu wa kiongozi huyo, Magufuli ana dhamira ya kuwatumikia na kuwahudumia Watanzania na ana uwezo wa kuwaweka pamoja Watanzania na kuhifadhi tunu ya amani.

Alitoa wito kwa wananchi wa Liwale wawakatae wagombea wachochezi na wazushi kwa kuwa hawafai na hawatajuta kumchagua Magufuli.

“Tunaenda kumchagua Rais, hatuendi kufanya mzaha, kura yako ni muhimu” alisema Majaliwa.

Alisema Magufuli alipanga kwenda Lindi Oktoba tano lakini siku iliyofuata alikuwa na mgeni Rais wa Malawi, Dk Lazarus Chakwera.

Alisema, wakati huo Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) ilikuwa imeshapanga ratiba za wagombea wote hivyo amelazimika kumtuma yeye aende kumuwakilisha na anaamini hakitaharibika kitu kwa kwa yeye (Majaliwa) ni msaidizi wake na wanakaa kuzungumza.

Majaliwa alisema, Magufuli anaipenda Lindi, atakwenda hadi Liwale na ana jambo lake kwenye mkoa huo. Alisema hayo wakati akimuombea kura Magufuli na wagombea ubunge na udiwani kupitia chama hicho.

Majaliwa alisema CCM ni taasisi yeye sera, uwezo wa kuziratibu changamoto za Watanzania nchi nzima.

Alisema serikali ya CCM imefanya kazi nyingi na nyingine zimewekwa kwenye mpango wa miaka mitano ndio maana anawaombea kura wagombea hao. “Watanzania bado tunayo dhamira ya kuwatumikia, kuwa wahudumu wenu, tumejipanga vizuri kushughulikia changamoto zetu kisekta,” alisema.

Aliwaambia wananchi wa Liwale kuwa Ilani ya uchaguzi ya CCM ina kurasa zaidi ya 14 zinazungumzia mkoa wa Lindi hali na kwamba hiyo inaonesha mapenzi aliyonayo Rais Magufuli kwa wana Lindi.

“Baada ya serikali kumaliza ujenzi wa barabara za makao makuu mikoani, sasa tunaanza ujenzi wa barabara za wilaya kwa wilaya. Lindi imepata bahati ya barabara nyingi kujengwa kwa kiwango cha lami”alisema.

Majaliwa alisema wananchi wanahitaji Rais ambaye anaweza kuhifadhi rasilimali za nchi, kuziratibu na kuziweka pamoja.

Alisema kabla ya Rais Magufuli kuingia madarakani Novemba 2015 nchi ilikuwa ikiibiwa madini, lakini alipoingia alifumua mikataba yote mibovu na kuirekebisha kwa maslahi ya nchi.

“Magufuli ameendelea kusimamia msimamo wake. Mrahaba wa madini sasa unajenga zahanati na vituo vya afya. Huyu ndiye rais tunayeenda kumpigia kura, huyu ndiye ninayemuombea kura John Magufuli”alisema na kuongeza; “Lazima tuambiane ukweli.

Lindi ni yetu, Liwale ni yetu, Kilwa ni yetu. Lazima tuelezane ukweli kwa manufaa yetu na mtakuja kunikumbuka,” alisema.

https://www.apps.tsn.go.tz/public/uploads/223964dcb4ca62e637bc1bf8434a3e3f.jpg

ZAIDI ya wataalamu wa afya ...

foto
Mwandishi: Lucy Ngowi

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi