loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Waliopata mimba likizo ya corona kufanya mitihani

BODI ya Mitihani ya Taifa Uganda (UNEB) imezitaka shule kuwasajili kufanya mitihani wanafunzi waliopata mimba wakati wa likizo ya kupambana na virusi vya corona. 

Kwa mujibu wa kalenda mpya, wanafunzi watafanya mitihani ya kupata cheti cha elimu cha Uganda (UCE) kuanzia Machi 1, mwakani, mitihani ya kumaliza elimu ya msingi (PLE) Machi 30 na cheti cha juu cha elimu Uganda (UACE) kuanzia Aprili 12, mwakani.

Akizungumza na waandishi wa habari mjini Kampala juzi, Katibu Mtendaji wa UNEB, Daniel Odongo alisema usajili wa wanafunzi ulianza Oktoba 22 mwaka huu.

Alisema usajili utafanyika kwa wiki tano na shule zote zimetakiwa kuhakikisha watahiniwa wote wanasajiliwa kwani hakutakuwa na muda wa nyongeza.

Alisema tofauti na ilivyozoeleka, mwaka huu usajili utafanyika kwa njia ya mtandao wa elektroniki njia wanayoamini itasaidia kufanya usajili kwa muda mfupi.

UNEB imeelekeza shule kusajili wanafunzi waliopata mimba wakiwa nyumbani kwenye likizo ya  kupambana na ugonjwa wa covid-19 kwani idadi ya wanafunzi waliopata tatizo hilo ni kubwa mwaka huu tofauti na miaka mingine.

SERIKALI  itatumia takriban  Faranga bilioni 75  kwa miaka ...

foto
Mwandishi: KAMPALA

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi