loader
Majaliwa: Tumieni fursa hii ya mara moja kwa miaka mitano

Majaliwa: Tumieni fursa hii ya mara moja kwa miaka mitano

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa ametoa wito kwa watanzania kutumia fursa inayotokea mara moja kila baada ya miaka mitano ya kupiga kura kuchagua viongozi wanaowataka.

Waziri Majaliwa amesema hayo mara baada ya kupiga kura katika Kata ya Nandagala Jimbo la Ruangwa mkoani Lindi na kusema kuwa kila mtanzania alipata nafasi ya kusikiliza sera za wagombea mbalimbali hivyo leo maamuzi yanabaki kwao.

“Tujitokeze kwa wingi kupiga kura kabla ya zoezi la uchaguzi kufungwa hapo saa kumi jioni  kutimiza haki zetu za msingi kikatiba” amesema Majaliwa.

https://apps.tsn.go.tz/public/uploads/e178b5ec6f9f84e4bcc1df2ec7ab6dd9.jpg

RAIS Samia Suluhu Hassan amehutubia taifa ...

foto
Mwandishi: Alfred Lukonge

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi