loader
Dstv Habarileo  Mobile
TPA
Picha

NGOME KUU CHADEMA ZANGUKA

CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), mpaka sasa ngome zake tatu zimeangushwa na Chama Tawala (CCM) katika majimbo ya Mbeya Mjini, Hai na Moshi Mjini.

Kuanguka kwa Mbowe ambaye alikuwa Kiongozi wa Kambi rasmi  ya upinzani bungeni na Mwenyekiti wa Chadema Taifa,  kwa mara ya kwanza chama hicho kinaenda kuongozwa na viongozi wa juu ambao sio wabunge.

Mwenyekiti Freeman Mbowe na Katibu wake John Mnyika wote sio wabunge.

Mbowe  ameangukia pua kwa kupata kura 27,684 dhidi ya mpinzani wake wa CCM Saashisha Mafuwe aliyeibuka kidedea kwa kupata kura 89,786

Kwa upande wa Mbeya Mjini jiimbo hilo lililokuwa ngome ya Chadema kwa miaka 10  likiongozwa na Joseph Mbilinyi ‘Sugu’  limechukuliwa na Tulia Ackson CCM ambaye ameshinda kwa kura 75,225 na kumshinda Sugu kwa kuwa 37,561

Akizungumza mara baada ya kutangazwa mshindi, Tulia alisema “Nawashukuru wana Mbeya kwa kunipa nafasi, kama binadamu kuna muda nilikasirika kutokana na wapinzani wangu maneno waliyokuwa wanatoa, tusameheane.

“Nipo tayari kushirikiana na kila mmoja kwa ajili ya kuleta maendeleo kwa wana Mbeya.

“Naamini yapo ambayo mpinzani wangu mkubwa angetamani kuyafanya iwapo angeshinda, nitashirikiana naye, nitamuomba ushauri, ili basi yale aliyotamani kuyafanya kwa ajili ya maendeleo ya wana Mbeya niyafanye mimi,” alisema

Jimbo la Moshi Mjini  Mgombea wa CCM, Priscus Tarimo ameshinda ubunge jimbo hilo kwa kupata kura 31,169 akifuatiwa na Raymond Mboya (CHADEMA) aliyepata kura 22,555.

Moshi Mjini kwa mara ya kwanza imechukuliwa na Chama tawala tangu mfumo wa vyama vingi uhasisiwe nchini Mwaka 1992 ambapo jimbo hilo limekuwa likitawaliwa na Chadema tangu mwaka 1995.

 

 

 

 

 

SERIKALI imewataka waliohujumu mali za vyama vya ushirika kujisalimisha ...

foto
Mwandishi: Vicky Kimaro

Post your comments

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi