loader
Dstv Habarileo  Mobile
TPA
Picha

FAHAMU 'VIGOGO' WA UPINZANI WALIONGUKA UBUNGE

WAGOMBEA kadhaa wa ubunge kupitia vyama vya upinzani wameanguka katika uchaguzi mkuu wa mwaka huu baada ya Tume ya Uchaguzi ya Taifa (NEC)  kutangaza ushindi kwa wagombea wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) dhidi ya viongozi hao wanaoongoza upinzani wa kisiasa nchini.

Wengi wao walikuwa wabunge ambao walikuwa wakitetea nafasi zao walizohuduma kwa miaka mitano na wengine zaidi ya kipindi hicho.

Vigogo waliopoteza majimbo hadi sasa;

HAI

Vigogo wa vyama hivyo vya upinzani akiwemo Kiongozi wa Kambi rasmi ya Upinzani katika Bunge la 11 na Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe wameshindwa kufurukuta katika uchaguzi huo uliofanyika jana Oktoba 28

Mbowe aliyekuwa akitetea jimbo la Hai ameangushwa kwa kupata kura 27,684 dhidi ya mpinzani wake Saashisha Mafuwe wa CCM ambaye amepata kura 89,786.

MBEYA MJINI

Joseph Mbilinyi ‘Sugu’ ameshindwa kutetea kiti chake cha ubunge jimbo la Mbeya Mjini baada ya kupata kura 37,561 dhidi ya mpinzani wake Tulia Ackson aliyepata kura 75,225.

TARIME VIJIJINI

Mbali na Mbowe, vigogo wengine waliongushwa ni hadi sasa ni aliyekuwa mbunge wa Tarime vijijini John Heche na jimbo hilo limenyakuliwa na Mwita Waitara wa (CCM)

Waitara ameshinda kwa kupata kura 35,758, dhidi ya Heche wa Chadema aliyepata kura 18,757.

IRINGA MJINI

Mchungaji  Peter Msigwa (Chadema) aliyeliongoza jimbo hilo kwa miaka 10, ameshindwa kulitetea baada ya msimamizi wa uchaguzi jimbo hilo kumtangaza Jesca Msambatavangu wa CCM kuwa mshindi wa ubunge wa jimbo hilo kwa kupata kura 36,034 huku Msigwa akipata kura  19,331

BUNDA MJINI

Ester Bulaya amepoteza Jimbo la Bunda Mjini baada ya kupata kura 13,258 dhidi ya mpinzani wake Robert Maboto CCM aliyepata kura 31,129

KIGOMA MJINI

Zitto Kabwe ameanguka katika Jimbo la Kigoma Mjini baada ya kudumu kwa miaka 28 tangu mwaka 1992 akiwa Mbunge wa Chadema kabla ya 2015 kushinda jimbo hilo kwa tiketi ya chama chake cha ACT - Wazalendo.

Msimamizi wa  uchaguzi wa jimbo hilo Mwalima Pangani, alimtangaza Kilumbe Ng'enda wa CCM kuwa mshindi wa Jimbo  hilo la  Kigoma Mjini baada ya kumuangusha Zitto Kabwe kwa kura  27, 688 huku Zitto Kabwe wa ACT- Wazalendo akipata kura 20,600. Mwailwa Pangani amesema kura zilizopigwa ni 50268.

TARIME MJINI

Pia aliyekuwa mbunge wa Tarime Mjini Esther Matiko ameshindwa kutetea nafasi yake baada ya kushindwa na mshindani wake, Michael Kembaki wa CCM.

ARUSHA MJINI

Aliyekuwa Mbunge wa jimbo la Arusha Mjini, Godbless Lema alipoteza kiti hicho kwa kupata kura 46,489 dhidi ya mpinzani wake, Mrisho Gambo aliyepata kura 82,480.

 

*Matokeo zaidi yataendelea kuletwa kwenu kupitia kurasa zetu za Instagram, Twitter na Facebook; @habarileo

SERIKALI imewataka waliohujumu mali za vyama vya ushirika kujisalimisha ...

foto
Mwandishi: Vicky Kimaro

Post your comments

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi