loader
Dstv Habarileo  Mobile
TPA
Picha

NEC yataja sifa za vyama kupata wabunge viti maalum

"Chama kitakachopata angalau asilimia  tano ya kura za wabunge  kitakuwa na  uhalali wa kupata  wabunge wa viti maalum,” ameeleza Mkurugenzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC)  Dk Wilson Mahera.

Akizungumza wakati akitoa taarifa fupi ya Uchaguzi Mkuu uliofanyika Oktoba 28, 2020, katika hafla ya kumkabidhi cheti mshindi wa kiti cha Urais, Dk Mahera amesema kuwa tayari NEC imeshatoa fomu kwa vyama vya siasa ili kupendekeza majina ya wabunge watakaopata nafasi ya kuwakilisha kupitia viti maalum na chama kitakachopata nafasi hiyo lazima kiwe na asilimia kuanzia tano za kura za wabunge.

Aidha ameongeza kuwa, "Tume ilitoa kibali cha utoaji wa elimu ya mpiga kura kwa asasi 245 kwa Tanzania bara na saba visiwani Zanzibar. Hata hivyo Tanzania inatumia mfumo ambao mgombea anaeyepata kura nyingi zaidi ndiye hutangazwa kuwa mshindi.”

SERIKALI imewataka waliohujumu mali za vyama vya ushirika kujisalimisha ...

foto
Mwandishi: Alfred Lasteck

Post your comments

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi