loader
Dstv Habarileo  Mobile
TPA
Picha

Mambosasa: Tunawashikilia Mbowe, Lema

KAMANDA wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, ACP Lazaro Mambosasa amesema wanawashikilia watu kadhaa wakiwemo viongozi wanne wa Chama cha Demokrasia na maendeleo (CHADEMA).

Viongozi wa Chadema wanaowashikilia ni pamoja na Freeman Mbowe ambaye ni mwenyekiti wa chama hicho taifa, Godbless Lema, Isaya Mwita (aliyekuwa Meya wa Dar) na Boniface Jacob (aliyekuwa Meya wa Ubungo).

Mambosasa amesema wanawashikilia viongozi hao kwa kuwa wanahatarisha usalama wa raia na mali zao kwa kuwa wamepanga kuandamana leo Novemba 02, 2020 kwa kuwatumia vijana kuchoma moto miundominu mbalimbali.

 Mapema juzi, Viongozi wa vyama vya ACT Wazalendo na Chadema walieleza umma kuwa wameandaa maandamano yatakayofanyika leo kwa lengo la kupinga matokeo ya Uchaguzi Mkuu.

SERIKALI imewataka waliohujumu mali za vyama vya ushirika kujisalimisha ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu

Post your comments

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi