loader
Dstv Habarileo  Mobile
JPM: Tutatekeleza, tutakuza uchumi na kutatua kero za wananchi

JPM: Tutatekeleza, tutakuza uchumi na kutatua kero za wananchi

RAIS John pombe Magufuli amesema atahakikisha anaendelea kusimamia rasilimali za taifa sambamba na kuendeleza mapambano dhidi ya rushwa

Rais Magufuli ameyasema hayo muda mfupi baada ya kuapishwa Mjini Dodoma leo Novemba 5, 2020 ikiwa ni awamu yake ya pili ya miaka mitano itakayomalizika mwaka 2025.

Amesema atahakikisha anasimamia maliasili na rasilimali za nchi na kukuza uchumi.

 “Nitaendeleza usimamizi wa mali asili, madini, rasilimali za majini, wanyamapori, mifugo na kadhalika.

“Sambamba na hilo tutatekeleza kwa namna kubwa katika kukuza uchumi na kushughulikia changamoto za umasikini zinazowakabili Watanzania. Ukosefu wa ajira kwa vijana na kero mbalimbali kwa wananchi,” amesema Rais Magufuli.

Rai Magufuli tayari ameiongoza Tanzania kwa awamu moja ambapo aliapishwa Novemba 5, mwaka 2015 na kuongoza kwa miaka mitano, kabla ya leo kuapishwa tena kuongoza awamu yake ya pili itakayofikia kikomo mwaka 2025.

foto
Mwandishi: Vicky Kimaro

1 Comments

  • avatar
    Gift Emmanuel
    05/11/2020

    Mungu akutangulie katika majukumu yako Dr JPM.

Post your comments

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi