loader
Dstv Habarileo  Mobile
Magufuli:  Uchaguzi umekwisha, tuchape kazi

Magufuli: Uchaguzi umekwisha, tuchape kazi

 “Uchaguzi umekwisha, uchaguzi umekwisha, uchaguzi umekwisha…

"…Uchaguzi sasa umekwisha, jukumu kubwa lililopo mbele yetu ni kuendeleza jitihada za kujenga na kuleta maendeleo kwa Taifa letu na niwahakikishie kuwa kiapo nilichoapa na alichoapa makamu wangu (Samia Suluhu Hassan), tutahakikisha tunakienzi kwa nguvu zote,” amesema Rais John Pombe Magufuli wakati akitoa hotuba yake mjini Dodoma muda mfupi baada ya kula kiapo cha kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Ras Magufuli amesema kuwa ni wakati sasa jukumu la kila mtu kuendeleza jitihada za kuiletea mafanikio Tanzania na kuenzi kiapo walichoapa.

Rais Magufuli “Kilichopo mbele yetu sasa ni kuenzi kiapo tulichoapa bila kujali itikadi zetu, dini, kabila, rangi.” amesema na kuongeza

“ Tutashirikiana na watu wote, kuhakikisha tunadumisha amani na utulivu, Muungano wetu wa Zanzibar tutauenzi lakini pia kuhakikisha tunatekeleza ahadi zote tulizotoa kipindi cha kampeni,” amesema Rais Magufuli

Aidha amesema ni kipindi cha kujenga taifa imara, kutekeleza miradi waliyoianzisha, na kukukuza uchumi ikiwa ni pamoja na kuhakikisha wanatatua changamoto za ukosefu wa ajira.

“Kuendeleza mapambano dhidi ya rushwa,ufisadi, wizi. Na mwisho wa uchaguzi ndio mwanzo wa uchaguzi mwingine,” amesema na kuushukuru umati wa watu uliojitokeza kushuhudia kuapishwa kwake.

foto
Mwandishi: Vicky Kimaro

Post your comments

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi