loader
Dstv Habarileo  Mobile
Museveni, Mnangagwa na simulizi za Afrika ya kujitegemea

Museveni, Mnangagwa na simulizi za Afrika ya kujitegemea

“Kawaida uwa sifuatilii mambo ya Tanzania, lakini kwenye uchaguzi nilikuwa nafuatilia, nilikuwa naweka TBC 1 naangalia muelekeo wa CCM kisiasa, hivi vyama vingine sijui muelekeo wake,” amesema Museveni na kushangilia na umati wa maelfu ya watu ambao walikuwa wakiimba CCM...CCM…CCM…ndani ya uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma.

Alisema, “Afrika kufaulu lazima tupongeze huu mwelekeo wa siasa, baada ya uhuru viongozi wengi wa Afrika walibadilika na kuwa vibaraka wa wazungu.

“Nyerere (Hayati Baba wa Taifa), Kenneth Kaunda (Zambia), Ian Khama (Botswana),  Ahmed Sékou Touré, (Guinea) Ahmed Ben Bella  (Algeria) Kwame Nkurmah (Ghana) Samora Machel (Msumbiji), ndio miongoni mwa viongozi wachache ambao hawakubadilika, walibaki na msimamo wao…

“…ewengine roho zao zilibadilika na mambo ya Afrika, wakawa vibaraka wa wazungu, leo tunaona wawakilishi kutoka Msumbiji, Zimbabwe hayo yote yametokana na msimamo wa Nyerere na wale wengine wachache.Tungefuata msimamo wa vibaraka leo hawa wote wasingekuja hapa,” amesema Museveni.

Amesema mwaka 2015 alikuwa na wasiwasi mkubwa endapo CCM ingeondolewa madarakani kutokana na vuguvugu kubwa la uchaguzi lililokuwepo wakati ule ambapo Chama Kikuu cha Upinzani Chadema, ilipomsimamisha Edward Lowassa ambaye alimeguka kutoka CCM na kwenda upinzani baada ya kuenguliwa katika kura za maoni, na CCM kumsimamisha Rais John Magufuli kwa mara ya kwanza kuwania kiti hicho cha Urais.

“Safari hii pia nilikuwa  nina hofu sana nikawa najiuliza hii itakuwaje , lakini nikaanza kusikiliza matokeo jimbo la Ilemela yule mama kashinda (Angelina Mabula), nikasikia Hai (Jimbo alililokua likiongozwa na Freeman Mbowe ) haya ndio majimbo ya awali yaliyotangazwa, nikasikia Newala, Mtwara nikasema basi tumeshinda,” amesema Museveni

“Vijana nawaona wengi sana hapa, mnatakiwa kurithi haya, nimekuwa mfuasi wa Mwalimu Nyeree kwa miaka 57 sasa.” Amesema na kuongeza kuwa mambo ya kuzingatia ni Ukombozi wa Afrika, kutoka kwenye kuomba na kujitegemea, na kuimarisha masuala ya ulinzi na usalama.

RAIS WA ZIMBABWE

Kwa upande wa Rais wa Zimbabwe Emerson Mnangagwa amesema Zimbabwe wanaitazamana Tanzania kama baba na mama wa Uhuru wao na kwamba Hayati Rais Nyerere alikuwa mzalendo wa kweli, na ndio maana hata sasa Mtanzania anayekwenda Zimbabwe wanamuona Nyerere

 “Mtu akija Zimbabwe akasema anatoka Tanzania, tunamuona kama Nyerere, Zimbabwe tunamshukuru sana Rais Magufuli alipokuwa mwenyekiti wa SADC alipigania Zimbabwe iondolewe vikwazo.

 “Tumewekewa vikwazo kwa muda mrefu sana miaka 10 imepita na sababu ni ndogo tu kuchukua ardhi yetu, Tanzania ndio imeonyesha njia kutaka ukanda wa SADC isimame kidete Zimbabwe tuondolewe vikwazo…

 “…Hata njaa kali ilipoingia nchini mwetu, Tanzania walitupatia mahindi, hata Uganda nao walituletea mahindi, ndio viongozi wazalendo kabisa katika ukanda wetu,” amesema Rais Mnangagwa

MAKAMU WA RAIS BOTSWANA

Makamu wa Rais wa Botswana Slumber Tsogwane kwa upande wake amesema Rais wan chi hiyo ameshindwa kuudhuria sherehe za uapisho wa Rais John Magufuli kwa kuwa kuna hotuba ya taifa lazima aitoe yeye.

 “Nitakuwa na fursa ya kuongea nawe Rais nikupe ujumbe maalum,” amesema

Amesema anapongeza wahasisi wa za Afrika akiwemo Hayati Mwalimu Nyerere na Jomo Kinyatta  ambao waliunda Umoja wa nchi zisizofungamana na upande wowote.

https://apps.tsn.go.tz/public/uploads/9342c18849ca0237e1ee8e2fe0c69a0d.jpg

OFISI ya Taifa ya Ukaguzi (NAOT) ni Taasisi ...

foto
Mwandishi: Vicky Kimaro

Post your comments

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi