loader
Dstv Habarileo  Mobile
TPA
Picha

Uchaguzi umekwisha, maisha yaendelee kwa amani

HAKUNA asiyekubali kwamba Mungu ametuvusha kwa amani na upendo mkubwa katika mchakato wa Uchaguzi Mkuu, uliofanyika Okotba 28 na kisha wateule kuapishwa kuwa viongozi kwa kipindi kingine.

Hatua ya kutambua kuwa ni Mungu aliyekuwa pamoja nasi ni ya muhimu sana, kwani uzoefu unaonesha kuwa katika mataifa mengi hiki huwa ni kipindi cha vurugu na machafuko, yanayosababisha vita ya wenyewe kwa wenyewe.

Hali hii kutotokea Tanzania, si kwamba ni wema au tuna ujuzi na kujiimarisha kwa ulinzi, bali ni msaada wa Mungu. Hivyo ni vyema kukubali kuwa washindi wameshinda na sasa maisha yanapaswa kuendelea.

Nafahamu kwamba katika uchaguzi huu, wagombea wa nafasi ya urais walikuwa 15 huku vyama 19 vyenye usajili wa kudumu vilishiriki uchaguzi kuanzia ngazi ya udiwani, uwakilishi, ubunge na urais.

Matokeo yaliyotangazwa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) kuwa Dk John Magufuli, aliyekuwa mgombea wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) ndiye mshindi wa kiti cha Rais na Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC) kumtangaza mgombea wa CCM, Dk Hussein Mwinyi kuwa mshindi wa nafasi hiyo Zanzibar, ndio mamlaka ya mwisho na ya juu kumtangaza mshindi wa nafasi hiyo.

Kutokana na ukweli huo wa Kikatiba, hakuna tunachosubiri tena, bali ni kurejea katika maisha ya kawaida ya kufanya kazi kwa bidii huku tukielekeza shukurani zetu kwa Mungu na kudumisha amani yetu kama walivyosisitiza viongozi wetu wa dini katika kongamano lao lililofanyika jana jijini Dar es Salaam. 

Walioshindwa ni vyema wakajipanga kwa ajili ya uchaguzi mwingine miaka mitano ijayo na kuwapa ushirikiano waliopo madarakani kwa sasa, kwani hata kama hawakubaliani nao, ndio waliochaguliwa na Watanzania wengi. Mungu Ibariki Tanzania na watu wake, Amina.

JANUARI mosi mwaka ujao Uganda itafanya uchaguzi mkuu kwa ...

foto
Mwandishi: Gloria Tesha

Post your comments

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi