loader
Majaliwa apitishwa na Bunge kwa asilimia 100

Majaliwa apitishwa na Bunge kwa asilimia 100

Bunge la Tanzania, limempitisha Mbunge wa Ruangwa, Kassim Majaliwa kuwa Waziri Mkuu kwa kupata kura zote 350 zilizopigwa na wabunge ambazo sawa na 100%.

Akizungumza bungeni jijini Dodoma hii leo, Majaliwa amesema amepanga kupita maeneo mbalimbali ya nchi kujionea shughuli za maendeleo zinazosimamiwa na wabunge.

“Tutapita katika majimbo yenu kukagua miradi mbalimbali  pamoja na kupata fursa ya kukutana na wananchi ili kusikiliza kero zao na kutafuta namna bora ya kuzipatia utatuzi” amesema Majaliwa.

Amesema atahakikisha maendeleo yanapelekwa katika majimbo yote hata kwa yale ambayo yanaongozwa na wapinzani. Amemshukuru Rais Magufuli kwa uteuzi wake na kuhaidi ushirikiano kwa Bunge.

https://apps.tsn.go.tz/public/uploads/937970746b415500b0ecacd9721a8250.jpg

RAIS Samia Suluhu Hassan amehutubia taifa ...

foto
Mwandishi: Alfred Lukonge

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi