loader
Son mchezaji bora Oktoba

Son mchezaji bora Oktoba

MSHAMBULIAJI wa Tottenham Heung-Min Son ametajwa kuwa mchezaji bora wa Ligi Kuu kwa Oktoba.

Mshambuliaji huyo wa Korea Kusini amefunga mabao manne Oktoba, ikiwemo kwenye ushindi wa mabao 6-1 dhidi ya Manchester United, Old Trafford na ushindi wa dakika za majeruhi wa Turf Moor dhidi ya Burnley, ulioifanya Tottenham ipande kileleni mwa msimamo wa Ligi Kuu.

“Mshambuliaji wa Tottenham Heung-Min Son yuko kwenye kiwango kimoja na Raheem Sterling, Sadio Mane na Mohamed Salah,” alisema Gary Neville

Mourinho amemuelezea Son, ambaye ana mabao manane na pasi mbili za mabao kwenye michuano yote msimu huu, kama mchezaji mwenye kiwango cha dunia msimu hadi msimu.

Son alijiunga na Tottenham akitokea Bayer Leverkusen mwaka 2015 na ametengeneeza uelewano mzuri na nahodha wake Harry Kane. Mourinho amekuwa akimpongeza mara kwa mara kutokana na uwezo wake anaouonesha kwenye mechi mbalimbali anazompa nafasi.

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 28 amebakiza miaka mitatu kwenye mkataba wake wa sasa na Tottenham na Mourinho anaamini klabu inaweza kufikia makubaliano kwa muda muafaka wa kumuongezea mkataba kwani anataka mchezaji huyo kuwa sehemu ya mipango yake ya muda mrefu.

https://apps.tsn.go.tz/public/uploads/ecba1cd6dbd8561d68dad395175f33c8.jpg

Klabu ya soka ya Chelsea imefikia muafaka ...

foto
Mwandishi: LONDON, England

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi