loader
Dstv Habarileo  Mobile
Serikali yaanzisha mfuko wa wasanii

Serikali yaanzisha mfuko wa wasanii

SERIKALI  imeanzisha mfumo  rasmi utakaowawezesha  wasanii kudai na kupata  haki zao stahiki kwa wakati.

Kauli hiyo ilitolewa kwenye viwanja vya  Bunge Jijini Dodoma jana na msemaji wa serikali na Katibu wa Wizara  ya  Habari, Utamaduni, Sanaa  na Michezo, Dk Hassan Abbas baada ya kusikiliza hotuba ya uzinduzi wa bunge la 12 iliyotolewa na Rais John  Magufuli.

Alisema atajitahidi  kutafsiri hotuba ya Rais Magufuli  kwa umakini na kuifanyia kazi ikiwemo kusimamia haki za wasanii kwa kuhakikisha wanatengeneza kazi bora.

“Rais tangu anaapishwa na leo (jana) nimesikia akizungumzia zaidi sekta ya sanaa kwa kuhakikisha tunawakuwa na wasanii ambao haki zao wanazipata,” alisema Abbas.

Alisema tayari mifumo wameshaianzisha kuhakikisha wasanii wanapata haki zao kirahisi kwa kuanzisha mfuko  ikiwemo Cosota kuhamishwa kwenda kwenye ofisi yake.

“Kubwa zaidi leo (jana) Rais ameongelea zaidi kuanzishwa kwa mfumo wa sanaa na utamaduni mfumo ambao wadau wataenda kuomba mikopo na kupata elimu umeshaanzishwa kinachosubiriwa ni utekelezaji tu,”alisema Abbas.

Alisema mipango waliyonayo ni kuboresha mifumo kwa kuwasaidia wasanii kupitia kazi zao  kuuza kwa tehama na kupata faida yao inayotakiwa.

https://apps.tsn.go.tz/public/uploads/26b6587e3312013e0f5e60a2109e9765.jpg

BAADA ya Yanga kuondolewa kwenye michuano ya Ligi ...

foto
Mwandishi: Tuzo Mapunda

Post your comments

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi