loader
Dstv Habarileo  Mobile
TPA
Picha

Yanga bado wamkomalia Morrison

KLABU ya Yanga imeliomba Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kupitia Kamati ya Nidhamu na Haki ya Wachezaji kusikiliza kesi waliyopeleka kuhusu Bernard Morrison Kabla ya dirisha dogo la usajili kufunguliwa.

Akizungumza Dar es Salaam jana Makamu Mwenyekiti wa Yanga, Fredrick Mwakalebela alisema TFF wanatakiwa kusikiliza kesi hiyo mapema kwa kuhofia timu iliyomsajili mchezaji huyo ( Simba ) wanaweza kutumia dirisha hilo kurekebisha matatizo waliyoyabainisha kwenye mkataba huo.

"Hatuna matatizo na TFF, ila tunachokiomba kesi yetu tuliyowapelekea isikilizwe mapema kabla ya dirisha dogo kufunguliwa kwa sababu Simba wanaweza kutumia nafasi hiyo kurekebisha kasoro zilizojitokeza kwenye mkataba huo," alisema Mwakalebela.

Pia wanaiomba TFF kusikilizwa kwa kesi ya mchezaji wao Ramadhan Kabwili ambayo tangu wameipeleka hawajapatiwa majibu.

"Kupitia kesi ya Kabwili tunaishukuru Taasisi ya Kupambana na Rushwa (Takukuru) kwa kuwapatia majibu baada ya kufanya uchunguzi sasa tunawaomba TFF nao wafanye hivyo Ili haki itendeke," alisema Mwakalebela.

Mwakalebela amewatoa hofu wanachama kuachana na propaganda zinazoendelea kwani sio za kweli na Yanga msimu huu wamejipanga kuchukua ubingwa.

"Timu zingine kama zina wasiwasi kuhusiana upangaji matokeo watoe vielelezo vya ushahidi," alisema.

Katika hatua nyingine mshauri mkuu wa Yanga, Senzo Mbatha alisema ripoti ya rasimu ya awali imekamilika na mwezi ujao wataalam kutoka Hispania wanatarajia kuja kuliweka wazi suala hilo.

"Ripoti ya kuelekea kwenye mabadiliko yanaenda vizuri na rasimu ya kwanza imekamilika na mwezi ujao wataalam kutoka Hispani watakuja kuwasilisha tayari kwa kuendeleza mchakato," alisema.

SERIKALI imewataka waliohujumu mali za vyama vya ushirika kujisalimisha ...

foto
Mwandishi: Tuzo Mapunda

Post your comments

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi