loader
Dstv Habarileo  Mobile
Forbes yaifagilia Tanzania kiutalii

Forbes yaifagilia Tanzania kiutalii

JARIDA la FORBES limeitaja Hifadhi ya Taifa ya Serengeti kuwa kivutio namba mbili kwa mwaka 2021 kati ya vivutio 21 vilivyoingia kwenye orodha hiyo duniani.

Jarida hilo maarufu limechapisha taarifa ya vivutio hivyo ikiwa ni siku chache baada ya Taasisi ya Kimataifa ya Ushauri wa Masuala ya Usafiri kwa watalii duniani ya Ovation ya Marekani, kuorodhesha vivutio 21, bora zaidi kwa kutembelewa mwaka 2021.

Katika ordha hiyo nchi tatu za Afrika zimeingia ambazo ni Tanzania ,Afrika Kusini na Rwanda na kuwa watalii waliotembelea vivutio hivyo awali wengi wametoa maoni yao kuvisifia na kushauri wengine kuvitembelea.

Hii inadhihirisha ushindi wa  hifadhi hiyo ambayo wiki iliyopita, ilishinda tuzo ya Taasisi ya Word Travel Awards (WTA) ya nchini Marekani ya kuwa hifadhi bora barani Afrika kwa mwaka 2020 kwa kuzipiku hifadhi nyingine tano barani humo.

Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi hiyo ya Utalii ya Ovation, Tina Rose alisema orodha hiyo ya vivutio imetokana utafiti wao wa jinsi wanavyofanikisha safari za watalii duniani kutembelea vivutio vya utalii na maoni yanayotolewa na wateja wao mara baada ya kutembelea vivutio hivyo.

“Wateja wetu wanatupa mrejesho baada ya sisi kuwashauri na kuwatajia vivutio na sifa zake, kisha wao kuchagua wapi watembelee na sisi kuwaunganisha, wakirudi hutoa mrejesho na watalii wengine wanaposoma huvutiwa na kutamani kwenda, katika vivutio 21 bora zaidi kwenda mwaka 2021, nchi ya Tanzania, Kisiwa cha Maldives na Antarctica zimo ndani’,alisema Rose.

Alisema kati ya vivutio hivyo 21, saba viko nchini Marekani na vingine viko katika nchi mbalimbali na kuwa namba moja imeshikwa na Kisiwa cha Maldives na kueleza sababu kuu ni uzuri wa kisiwa hicho chenye fukwe safi na zenye mvuto sambamba na hali ya hewa nzuri.

Hifadhi ya Taifa ya Serengeti iko kwenye kivutio namba mbili kati ya hivyo 21 vya kutembelewa mwaka 2021 . Inatajwa kuwa mfumo wa ikolojia wa hifadhi hiyo, kuhama kwa wanyama na mambo mengi yanayohusu hifadhi hiyo yamevutia watalii na hivyo kuendelea kuwa kivutio kwa mwaka 2021.

“Hifadhi ya Serengeti ina mengi ya kuvutia, mfumo wa ikolojia wake, kuhama wa misafara mirefu na wanyama wengi wakiwamo nyumbu bado kunaendelea kushangaza dunia,nyika zake, mito iliyomo na vitu vingi vya kitalii vinaifanya hifadhi hiyo ambayo ni miongoni mwa maajabu saba ya asili ya Afrika, bado inavutia sana watalii,’’alisema Joyce Novick Mshauri kutoka Taasisi hiyo ya Ovation .

Alisema uoto wa hifadhi hiyo imekuwa sehemu muhimu ya malisho kwa Wanyama kutokana na ukweli kuwa ina mandhari ya kuvutia na yenye nyika fupi ambayo wanyama mbalimbali wanaipenda wakiwamo simba,pundamilia,swala, nyati,tembo, chui na wengine kama sehemu yao muhimu ya kupata chakula.

Namba tatu ni barafu iliyoko Antarctica,Namba nne ni  Ziwa  Powell,lililoko  Utah, tano ni Jackson Hole,Wyoming ,sita ni Cusco,Peru ambalo ni eneo la kiistoria,saba ni Hifadhi ya Sokwe iliyoko Kigali, Rwanda.

Vivutio vingine ni Hifadhi ya Taifa ya Denali,Alaska, Fukwe ya Porto Cervo,Italia, Sonoma-Count,Califonia,Uoto wa asili wa Norwegian Fjords, Milima ya Great Smoky  -Tenessee, Makabi ya kihistoria ya Kyoto,Japan na Fukwe ya Gansbaai ya Afrika Kusini.

Vingine ni Mapango ya Queen Stown-New Zealand, Hifadhi ya Taifa ya Acadia-Maine, Umbria-Italia, Merida-Mexico, Kisiwa cha Lombok -Indinesia nae neo la Bluffton Carolina Kusini.

https://apps.tsn.go.tz/public/uploads/26e86258d024d115e1ed7b14c4986ed5.jpg

WIZARA ya Kilimo imesema Desemba mwaka huu ...

foto
Mwandishi: Ikunda Erick

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi