loader
Dstv Habarileo  Mobile
TPA
Picha

Yanga yapata Katibu mpya

KLABU ya Yanga kupitia kwa Makamu Mwenyekiti, Fredrick Mwakalebela imemtangaza rasmi Haji Mfikirwa kuwa kaimu Katibu Mkuu wa timu hiyo kwa muda Hadi hapo watakapo ziba nafasi hiyo.

Mfikirwa ambaye ni Mkurugenzi wa Fedha na Utawala kwenye timu hiyo amechukua nafasi hiyo siku chache tangu kusimamishwa kazi kwa mwanasheria, Saimon Patrick aliyekuwa akikaimu nafasi hiyo.

Simon alisimamishwa na uongozi wa timu hiyo kupisha kamati iliyochaguliwa na uongozi wa Yanga kuchunguza ukweli wa tuhuma zinazomkabili za kuihujua Yanga.

Akizungumza Dar es Salaam jana, mara baada ya uteuzi huo Mwakalebela alisema Yanga ina mipango na shughuli nyingi wameziba nafasi hiyo kuhakikisha kazi zinaendelea muda wote.

Kwa upande wake, Mfikirwa amewashukuru viongozi wa Yanga kwa kuendelea kumuamini na kumpatia nafasi kubwa ya kiutendaji wa shughuli zote za klabu.

Alisema ana jukumu kubwa la kufanya, kwanza kusimamia suala la mchakato wa mabadiliko, ambalo ni wimbo kwa mashabiki na wanachama wote wanatamani kuona timu yao inajiendesha kwa mfumo wa kisasa.

TIMU ya Taifa ya Tanzania kwa wachezaji wenye umri ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu

Post your comments

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi