loader
Dstv Habarileo  Mobile
TPA
Picha

Tanzania kuendelea kuisaidia Congo kurejesha amani

SERIKALI imeahidi kuendelea kuisaidia Congo kuhakikisha changamoto za  ulinzi na usalama zinazoikabili nchi hiyo zinatatuliwa ili kuimarisha hali ya amani katika ukanda wa maziwa makuu.

Hayo yamesemwa na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Profesa Palamagamba Kabudi  alipokuwa akimwakilisha Rais John Magufuli katika mkutano wa nane wa kawaida wa wakuu wa nchi na Serikali wa Jumuiya ya Nchi za Ukanda wa Maziwa Makuu (ICGLR) uliofanyika kwa njia ya video.

"Tanzania tutaendelea kusaidia juhudi za kuimarisha ulinzi na usalama katika eneo la mashariki mwa Congo - DRC kwani kukosekana kwa utulivu wa kisiasa na kiusalama kwa nchi hiyo kunahatarisha usalama wa eneo lote la Jumuiya nzima ya ICGLR," alisema Kabudi.

Alisema kuwa Congo Brazaville ilikuwa ikikabiliwa na uasi kutoka kundi la Ninja lililokuwa  likiisumbua serikali  kwa miaka mingi hata hivyo hadi kufikia katikati ya mwaka 2019 uasi ulitulia kufuatia mazungumzo ya kusitisha  mapigano kati ya kundi hilo na Serikali.

Alisema Congo-Kinshasa na Congo-Brazaville ni muhimu katika eneo la maziwa makuu kutokana na kuwepo kwa asilimia kubwa ya rasilimali za misitu, maji na madini ambavyo vinahitajika sana duniani na kuongeza kuwa umuhimu zaidi unahitajika kutokana na ukweli kuwa kuna haja kubwa ya kutunza mazingira, kuzalisha nishati na kukuza uchumi wa dunia.

Aliongeza kuwa kukosekana kwa utulivu wa kisiasa na kiusalama katika nchi hizi kunahatarisha usalama wa eneo lote la Maziwa Makuu ikiwamo na usalama wa dunia kutokana na uwezekano wa baadhi ya mataifa makubwa kugombea rasilimali hizo.

Mkutano huo wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Jumuiya ya ICGLR umepokea na kujadili taarifa mbalimbali kuhusu jumuiya hiyo , mbali na hali ya kisiasa na kiusalama katika ukanda huo.

Pia umeangalia pia suala la michango ya wanachama katika bajeti ya Sekretariati na Mfuko Maalumu wa maendeleo, taarifa ya mkutano wa Mawaziri wa Mambo ya Nje wa Jumuiya, taarifa ya mkutano wa Mawaziri wa Ulinzi  kuhusu hali ya usalama wa Ukanda wa Maziwa Makuu na taarifa ya mkutano wa Mawaziri wa Afya.

Nchi wanachama wa ukanda wa maziwa makuu ni pamoja na Angola, Burundi, Jamhuri ya Kati, Demokrasia ya Kongo, Jamhuri ya Kongo, Kenya, Rwanda, Sudan, Sudani Kusini, Tanzania, Uganda na Zambia.

Oktoba 2019, mkutano wa wakuu wa Nchi wa Jumuiya ya Nchi za Ukanda wa Maziwa Makuu ulifanyika nchini Congo Brazzaville.

Wakati huo huo, Profesa Kabudi amekutana na kumuaga Mwakilishi Mkazi wa Benki ya Maendeleo Afrika (AfDB),Alex Mubiru ambapo pamoja na mambo mengine amemshukuru Mubiru kwa mema aliyoyafanya nchini hasa katika kuhakikisha kuwa Tanzania inapiga hatua kimaendeleo.

SERIKALI imewataka waliohujumu mali za vyama vya ushirika kujisalimisha ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Maalumu

Post your comments

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi