loader
Dstv Habarileo  Mobile
TPA
Picha

Watumishi Mambo ya Ndani waagizwa kuzingatia viapo

KATIBU Mkuu, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Christopher Kadio amewataka watumishi wa wizara hiyo kuzingatia viapo vyao katika utumishi ili Watanzania wapate huduma inayostahili.

Kadio alitoa rai hiyo jijini hapa wakati wa akizindua baraza dogo la wafanyakazi katika wizara hiyo.

Alisema kwa watumishi hao kuzingatia viapo vyao vya utumishi kutawafanya kuhudimia wananchi huduma ipasavyo kwa kuzingatia haki na usawa.

"Huu ni wakati wa Watanzania kupatiwa huduma bora zenye viwango na kuwataka kila mmoja kufanya kazi kwa bidii na maarifa bila kumwangalia mtu mwingine,” alisema.

Kadio pia aliagiza wafanyakazi kutunza na kuzisimamia vema mali walizokabidhiwa kwani kufanya hivyo ni kutekeleza malengo yake aliyopangiwa na mkuu wake wa kazi lakini kinyume chake ni kujiweka kwenye hali ngumu ya kiutumishi.

Pia amewataka Watumishi katika Wizara hiyo kubuni mbinu za kuongeza katika ukusanyaji wa maduhuli kwani bado kuna mianya mingi ambayo inapoteza fedha za serikali bila sababu za msingi.

Mwenyekiti wa baraza hilo Emmanuel Kayuni alisema wameamua kuitisha baraza hilo pamoja na mambo mengine wapangiane mikakati ya kuongeza maduhuli pamoja na kuona namna bora ya kuboresha utendaji kazi kwa mtu mmoja mmoja.

Ofisa huduma za uangalizi mkoa wa Dar e Salaam, Mwanaidi Makongo alisema maagizo ya Katibu mkuu hayapaswi kujadiliwa badala yake yanaihitaji utekelezaji wa vitendo ili kuifikia ndogo ya upatikanaji wa huduma bora kwa wateja.

SERIKALI imewataka waliohujumu mali za vyama vya ushirika kujisalimisha ...

foto
Mwandishi: Anastazia Anyimike, Dodoma

Post your comments

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi