loader
Dstv Habarileo  Mobile
TPA
Picha

Mgunda:Tanzania haina wachezaji warefu wa kike

KOCHA wa timu ya Taifa ya vijana ya mpira kikapu, Bahati Mgunda amesema Tanzania ina uhaba wa wachezaji warefu wa kike.

Mgunda, anayefundisha timu ya CRDB inayoshiriki michuano ya CRDB Taifa Cup amesema katika miaka ya nyuma, timu za Tanzania zilikuwa na wachezaji wengi wa kike warefu, lakini katika miaka ya hivi karibuni, wachezaji hao ni wachache sana.

Mgunda, ambaye pia ni kocha mkuu wa timu ya vijana ya kombaini ya Afrika, amesema kuna faida nyingi kwa mchezaji wa mpira wa kikapu kuwa mrefu na urefu ni moja ya sababu ya timu kushinda.

Akitaja baadhi ya faida hizo, Mgunda alisema faida hizo ni pamoja na mchezaji kuwa karibu na nyavu kwa ajili ya kutumbukiza mpira ili kupata pointi.

“Mchezaji akiwa mrefu, ana uwezo wa kuruka juu kidogo tu na akafunga kwa urahisi” alisema

Mgunda, aliyeipeleka timu ya kombaini ya Afrika katika michuano ya dunia iliyofanyika mwaka jana katika mji wa Orlando nchini Marekani alisema faida nyingine ni pamoja na uwezo wa kuchukua ‘rebounds’.

Lakini pia alisema anakuwa na uwezo wa kutibua mpira ambao unataka kuingia nyavuni kwa kuupiga nje na kitendo hiki mara nyingi kinafurahiwa na mashabiki kwa kupiga kelele kila kinapotokea.

Amesema katika miaka ya nyuma, wachezaji kama Grace Daudi ‘Sister’, ambaye kwa sasa ni marehemu, walikuwa na urefu huo unaohitajika na uwezo akiwa uwanjani , ndio maana walikuwa wakichaguliwa pia katika michezo mingine kama vile netiboli.

Alisema sio vibaya kwa wachezaji wafupi kucheza mchezo huo, lakini wanalazimika kuwa na vitu vya ziada ili wafanye vizuri.

 “Tunao wachezaji wafupi, hata kwa upande wa wanaume, lakini wengi wao utakuta wana vitu vya ziada na wamekuwa wakifanya vizuri.

Mgunda alisema kuna haja ya makocha kuanza kutafuta wachezaji wa kike warefu wanaopatikana hasa katika mikoa ya kanda ya ziwa.

Mwaka juzi nilikwenda Magu, mkoani Mwanza na nikakuta wachezaji warefu mashuleni, ambao wanapenda wawe wachezaji lakini hawajui pakuanzia.

Anasema alifanikiwa kurudi Dar es Salaam na wachezaji hao wawili mapacha wa kike na kiume ambao, kwa sababu ya kucheza kikapu, wamepewa msaada wa kusoma bure na shule ya sekondari ya High View iliyopo Gongolamboto, wakiwa kidato cha tatu.

TIMU ya Taifa ya Tanzania kwa wachezaji wenye umri ...

foto
Mwandishi: Suleiman Jongo, Dodoma

Post your comments

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi