loader
Dstv Habarileo  Mobile
TPA
Picha

Kidunda amtambia Mbelwa

BONDIA wa ngumi za kulipwa Seleman Kidunda ametuma salamu kwa mpinzani wake Said Mbelwa na kumueleza kuwa yeye sio mtu wa mchezo na wala hatanii akimtaka ajiandae kabla ya kukutana naye.

Kidunda ni miongoni mwa mabondia 16 watakaopanda ulingoni katika pambano la utangulizi la kumsindikiza pambano kuu kati ya Idd Pialari dhidi ya Mfilipino Arnel Tinampay,  Novemba 28, katika ukumbi wa Next Door Arena.

Akizungumzia maandalizi yake Dar es Salam jana,  Kidunda alisema yeye ni bondia mzoefu ambaye kabla ya kuingia kwenye ngumi za kulipwa alikuwa kwenye ridhaa na anajivunia kucheza mapambano mengi katika nchi mbalimbali duniani.

“Nimeingia kwenye ngumi za kulipwa kuwaelekeza namna ya kupigana kwa sababu nina uzoefu na nimekutana na mabondia wengi duniani, namweleza Mbelwa kuwa mimi sitanii nampiga kweli,”alisema bondia huyo wa zamani wa timu ya taifa ya ndondi.

Mbali na yeye, wengine waliotajwa na promota wa pambano hilo Seleman Semunyu ni Lulu Kayage atakayechuana dhidi ya Stumai Muki, Adam Yusuph dhidi ya Adam Kipenga, Shedrack King’asti dhidi ya Vicent Mbilinyi.

Wengine ni Ismail Galiatano dhidi ya Mustapha Dotto, Salehe Mkalekwa dhidi ya Ramadhan Shauri na Imani Mapambano dhidi ya Japhet Kaseba.

Semunyu alihimiza mashabiki wengi kujitokeza kwa wingi siku hiyo ili kuweka historia ya kujaza ukumbi.

Alisema anajivunia kupitia Kampuni ya Peak time Media ni miongoni mwa waliochangia kupandisha hadhi mchezo huo kwa kuutoa uswahilini na kuupeleka sehemu zenye hadhi ambazo wengi wanaweza kufika.

TIMU ya Taifa ya Tanzania kwa wachezaji wenye umri ...

foto
Mwandishi: Grace Mkojera

Post your comments

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi