loader
Dstv Habarileo  Mobile
TPA
Picha

Tanzania kutopokea misaada, mikopo inayovunja utu- Prof Kabudi

WAZIRI wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Profesa Palamagamba Kabudi amesema Tanzania haitakubali kudhalilishwa utu na heshima yake kama nchi huru,  kupigishwa magoti kupata misaada na mikopo kutoka katika nchi yoyote duniani.

Akizungumza na wafanyakazi wa wizara ikiwa ni mara ya kwanza tangu alipoteuliwa kuongoza wizara hiyo, alisema Tanzania ipo tayari kushirikiana na nchi yoyote itakayoheshimu na kujali uhuru wake.

"Never Never (hapana) hatutaruhusu mikopo na misaada ambayo inadhalilisha nchi, hakuiruhusu wakati wa Mwalimu Julius Nyerere haitaruhusu katika utawala huu wa sasa," alisema.

Alisema Tanzania haijawahi kupigishwa magoti kwa ajili ya kupokea misaada na mikopo yenye masharti ya kudhalilisha nchi tangu wakati wa Mwalimu Nyerere.

"Alivunja uhusiano wa ubalozi wa Uingereza nchini 1965-1972 na kurudisha pauni milioni tano, pia alivunja uhusiano wa kibalozi na Ujerumani 1964 kwa kulazimisha kuvunja muungano wa Bara na Zanzibar na kurudisha fedha za nchini hiyo milioni 35 kutokana na kutaka nchi kukubali masharti yao,” alisema Kabudi.

“Nchi itasimamia heshima yake na haitapokea misaada na mikopo ambayo inavunja utu waje. Kati ya fedha na misaada, tutasimamia utu wetu. Hatutakubali kudharauliwa…sisi ni binadamu na tupo sawa na tupo tayari kuwasikiliza na kushirikiana kama yapo yaliyopungua kwao na kwetu kujadiliana."

Profesa Kabudi alisema nchi itashirikiana na wote walio tayari kushirikiana nayo kuzungumza kama kuna upungufu kwao na nchini, lakini hawatakuwa na mjadala kwa nchi itakayotaka kudhalilisha utu na heshima ya nchi.

Alisema Tanzania ipo tayari kujadiliana, kushauriana na haichagui rafiki na inakaribisha urafiki kutoka pande zote za dunia .

Alimwagiza Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, kuhakikisha kila balozi nchini inapata ilani ya uchaguzi na hotuba ya Rais John Magufuli ya kufungua Bunge la 12 Novemba 20 mwaka huu pamoja na ya kufunga Bunge aliyotoa Juni 16. Ameagiza pia wawe na waraka aliotoa Nyerere mwaka 1969 kwa watumishi wa ofisi ya Rais mambo ya nje.

Waziri Kabudi aliwashukuru watendaji wa wizara hiyo ambao katika kipindi cha miaka mitano wamechangia kupata mafanikio makubwa yakiwamo ya kufungua balozi mpya tano na pia imeimarisha na kuongeza fursa za uwekezaji kupitia diplomasia ya biashara kwa kushawishi wawekezaji kuja nchini.

Alitoa mfano wa namna wawekezaji walivyobadili mkoa wa Simiyu kutokana na mabalozi wa Tanzania nchni Malaysia na Singapore, Ramadhan Dau na Elizabeth Kione wa Uturuki kupeleka wawekezaji katika mkoa huo na mikoa mingine.

Aliwataka wafanyakazi wa ziara hiyo kusoma Ilani ya Uchaguzi yenye kurasa 303 kuangalia maeneo yanayowahusu na mengine wanayoweza kusaidia kuwezesha, kushauri na kutekeleza moja kwa moja.

Miongoni mwa mambo ambayo ilani ya Uchaguzi imeagiza ni kuhusu diplomasia ya uchumi kwa kutaka wizara na mabalozi kuongeza kasi ya kufanya uchumi na kuweka mikakati ya kuendeleza biashara ya Tanzania na nchi jirani.

Katibu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki,  Wilbert Ibuge alisema wakati huu si wa kupeana raha ni kuchapa kazi kwa kasi na kujituma.

SERIKALI imewataka waliohujumu mali za vyama vya ushirika kujisalimisha ...

foto
Mwandishi: Magnus Mahenge, Dodoma

Post your comments

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi