loader
Dstv Habarileo  Mobile
TPA
Picha

Mama Samia mgeni rasmi NBC Marathon

MAKAMU wa Rais Samia Suluhu Hassan anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika mashindano ya NBC Marathon yatakayofanyika leo Jijini Dodoma na atashiriki mbio za kilomita 5.

Hayo yamesemwa na Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Michezo Dk Yusuph Singo wakati wa mkutano na waandishi wa habari uliolenga kueleza  hatua iliyofikiwa katika maandalizi ya mashindano hayo.

“Lengo la mashindano ya NBC Marathon ni kuchangisha fedha za  kusaidia  mapambano dhidi ya ugonjwa wa kansa ya shingo ya kizazi katika hospitali ya Ocean Road ya jijini Dar es Salaam” alisema Dk Singo.

Mashindano hayo yatashirikisha wanariadha 3000 katika mbio za kilomita 5, 10, 21 na 42 ambapo jumla ya Sh. Milioni 45.4 zitatolewa kama zawadiwa kwa washindi.

Kwa upande wake, Meneja Mahusiano wa Benki ya NBC, William Kallaghe alisema kuwa maandalizi ya mbio hizo yamekamilika na njia zote zitakazotumika kwa mashindano hayo zimetambuliwa na kuthibitishwa na Shirikisho la Riadha kwa kukidhi vigezo  na wamepewa cheti.

“NBC ipo makini na mashindano haya na imeingia mkataba wa miaka mitano kudhamini mashindano haya ambapo mapato yanayotokana na usajili wa wanaridha zote zitaelekezwa hospitali ya Ocean Road kuwahudumia wagonjwa wanaosumbuliwa na tatizo la kansa ya shingo ya kizazi” alisema Kallaghe.

Mashindano hayo yatashirikisha pia wanariadha kutoka Kenya, Malawi na Uganda ambapo washiriki hao 35  wote wamefanyiwa vipimo vya Covid-19.

 

SERIKALI imewataka waliohujumu mali za vyama vya ushirika kujisalimisha ...

foto
Mwandishi: Na Mwandishi Wetu

Post your comments

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi