loader
Dstv Habarileo  Mobile
Urusi yawawekea vikwazo  wawakilishi 25 wa Uingereza

Urusi yawawekea vikwazo wawakilishi 25 wa Uingereza

URUSI imeanzisha zuio kwa wawakilishi 25 wa Uingereza kutoingia nchini humo kuhusiana na vikwazo vya Uingereza kwa kile kinachoitwa kesi ya Magnitsky.

Hayo yalibainishwa mwishoni mwa wiki na Mwakilishi wa Wizara  ya Mambo ya Nje wa Urusi,  Maria Zakharova.

“Katika kujibu vitendo visivyo vya kirafiki vya Mamlaka za Uingereza na kwa kuzingatia msingi wa kanuni za nchi, upande wa Urusi umefanya uamuzi wa kuweka vikwazo binafsi dhidi ya wawakilishi 25 wa Uingereza ambao wamezuiwa kuingia katika Shirikisho la Urusi,” alisema Zakharova.

Kutokana na hilo, alitoa wito kwa Uongozi wa Uingereza kuachana na makabiliano yasiyo na sababu dhidi ya Urusi. “Hatua zozote zisizo za kirafiki hazitabaki bila majibu yanayowiana,”alisema.

Julai 6 mwaka huu, Uingereza ilitangaza vikwazo binafsi dhidi ya raia 25 wa Urusi ambao Uingereza inadhani walihusika na uvunjifu wa haki za binadamu.

https://apps.tsn.go.tz/public/uploads/c1b7e5652690aaa99cd8288b263571f2.jpg

KAMPUNI ya Qnet imezindua ...

foto
Mwandishi: MOSCOW, Urusi

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi