loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Kidato cha 4 waanza mtihani, shule 71 zaonywa

WANAFUNZI wa kidato cha nne leo wanaanza mtihani wa taifa na Baraza la Mtihani la Taifa (NECTA) likivionya vituo 71 vya mtihani vilivyoripotiwa kujipanga kufanya udanganyifu.

 NECTA imesema, wanafunzi 490,103 wanatarajiwa kuanza mtihani huo na Mtihani wa Maarifa (QT) na kwamba, unatarajiwa kumalizika Desemba 11 ikihusisha watahiniwa 448,164 wa shule na 41,939 wa kujitegemea.

Katibu Mtendaji wa NECTA, Dk Charles Msonde (pichani) alisema jijini Dar es Salaam kuwa, miongoni mwa watahiniwa wa shule 213,553 ni wavulana, wasichana ni 234,611 na kwa watahiniwa wa QT wako 9,426. Dk Msonde amezionya shule 71 zinazodaiwa kupanga udanganyifu kuwa zisithubutu kufanya hivyo.

Alitoa onyo hilo jijini Dar es Salaam wakati akitangaza matokeo ya mtihani wa taifa wa darasa la saba uliofanyika Oktoba mwaka huu.

Alisema NECTA imepata taarifa kuwa shule 71 za sekondari zimepanga kufanya udanganyifu huo. Alitaja shule hizo ambazo ni vituo vya mtihani kama vilivyoorodheshwa hapo chini majina ya kituo cha mtihani na mahali ilipo kwenye mabano.

 Sekondari ya Wavulana ya Bwiru, Sekondari ya Baptist Deasiz za (Mwanza), Shule ya Sekondari Kiranyi (Arusha), Shule ya Sekondari Ihumwa (Dodoma), Shule ya Sekondari Golden Ridge (Geita), Shule ya Sekondari Geita-Adventist (Geita).

Nyingine ni Shule ya Sekondari ya Wavulana Waja (Geita), Shule ya Sekondari Nyamala, Lyanika, Mufindi Girls, Regina Pachi Girls zote za (Iringa), Shule ya Sekondari Rusumo (Kagera), Shule ya Sekondari St Fransisco (Kigoma), Sekondari ya Songwe Sunrise (Songwe).

Katika orodha hiyo Mkoa wa Kilimanjaro jumla ya shule 11 za sekondari zimeripotiwa kupanga kufanya udanganyifu huo ikiwemo Seminari ya Agape Junior, St Mary Goret, Ebenezer Sango, Minja Technical, Minja Sekondari, Nyerere Sekondari, SEUTA Sekondari, Greenbird Sekondari, Mema Sekondari, Oshara Sekondari na Sanya Juu Sekondari.

 Mkoa wa Mara umetajwa kuwa na shule 11 zinazotuhumiwa kupanga kufanya udanganyifu kwenye mtihani huo ikiwemo Mugumu Sekondari, Nyeruma Sekondari, Kukirango Sekondari, Bumangi Sekondari, Kemoramba, Musoma Utalii Sekondari, Erato Sekondari, Mwembeni Sekondari, Morembe Sekondari, Marshi Sekondari na Paroma Sekondari.

Mkoa wa Kusini Pemba shule tatu zimetajwa kupanga kufanya udanganyifu nazo ni Fidel Castro Sekondari, Shamiani Sekondari na Madungu Sekondari.

Wakati Mkoa wa Mjini Magharibi shule mbili zimetajwa nazo ni Zanzibar Comercial Sekondari na Philter Federal Sekondari. Mkoa wa Mbeya shule nane zimetajwa katika orodha hiyo nazo ni Itundu Sekondari, Swila Sekondari, Onicah Sekondari, Wenda Sekondari, Mpesu Sekondari, Ntonzo Sekondari, St Marcus Sekondari na Kipoke Sekondari.

Mtwara shule mbili zimetajwa nazo ni Vihokoli Sekondari na Mpotwa Sekondari wakati Mkoa wa Morogoro shule zake tatu zimetajwa ikiwemo Mkono wa Mara, Bokela Sekondari na St Peter Seminari. Mkoa wa Ruvuma shule zake 10 zimetajwa nazo ni Nanungu Sekondari, Mtakanini Sekondari, Magazini Sekondari, Luna Sekondari, St Paul Liuli ,Kilumba Sekondari, Mango Sekondari, Matogoro Sekondari, Sasawala Sekondari na Peramiho Girls.

 Mkoa wa Simiyu nao umetajwa kwenye orodha hiyo ambapo shule saba zimo kwenye tuhuma hiyo nazo ni Bariadi Sekondari, Simiyu Sekondari, Kusekwa Memorial Sekondari, Mhunze SekondariIpililo Sekondari, Shishiyu Sekondari na Kulimi Sekondari.

 Dk Msonde aliwataka wakuu wa shuke tajwa na wasimamizi wote wa mitihani kutothubutu kutekeleza njama hizo kwani watakaobainika hatua kali zitachukuliwa dhidi yao.

 “Narudia tena kuwaonya wakuu wa shule na wasimamizi wote wa mitihani kutodiriki kutekeleza mpango huo ovu wa udanganyifu, tukiwabaini tutachukua hatua kali,” alisema. Aliwataka watahiniwa wasikubali kupewa majibu na walimu ama wasimamizi wa mitihani kwani wakibainika watafutiwa matokeo na kuwataka watoe taarifa za udanganyifu kwa simu namba 0738 971989 au 0735 540729.

Mtaalamu wa Lishe ya Binadamu kutoka ...

foto
Mwandishi: Na Ikunda Erick

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi