loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

ADA-Tadea wataka wapinzani kumuunga mkono Dk Mwinyi

MWENYEKITI wa Chama cha ADA Tadea, Juma Ali Khatib amewataka viongozi wa vyama vya siasa kumuunga mkono Rais wa Zanzibar, Dk Hussein Mwinyi ili kutekeleza ahadi alizozitoa wakati wa kampeni zake za kuleta maendeleo ya kiuchumi.

Akizungumza na waandishi wa habari jana mjini Unguja, alisema uchaguzi umekwisha na sasa ni kufanya kazi na kuachana na siasa za chuki na uhasama.

Aliwataka viongozi wa vyama vya siasa kuweka maslahi ya nchi kwanza, badala ya kuwa na maslahi yao binafsi kwa sababu vyama na viongozi wa vyama vya siasa watakufa lakini Zanzibar itakuwepo.

Aliwataka wanasiasa kutii maridhiano ya Serikali ya Umoja wa Kitaifa ambapo Dk Mwinyi alishaahidi maridhiano hayo kuyatekeleza kwa vitendo ikiwemo kuteua wizara mbili za wapinzani ambazo zimeachwa zikiwasubiri wapinzani kuingia katika baraza la wawakilishi.

"Namfahamu Maalim Seif (Shariff Hamad wa ACT-Wazalendo) ni mwanasiasa wa maridhiano hivyo kutii agizo la Rais katika kutekeleza maridhiano hayo zaidi kwa faida ya Wazanzibari kwa sababu maendeleo hayana chama,"alisema Khatib.

Pia alisema chama hicho kimefurahi na mwenendo wa Dk Mwinyi aliouanza na kuwataka mawaziri walioteuliwa kutekeleza maagizo 13 waliyoagizwa baada ya hafla ya kuwaapisha mawaziri hao.

Alimpongeza Dk Mwinyi kwa kumteua Hemed Suleiman kuwa Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar na kumuelezea kiongozi huyo kuwa ni mchapa kazi hodari na wakati alipokua Mkuu wa Mkoa wa Kusini Pemba alifanikiwa kuokoa Sh bilioni 3.5 za  karafuu zilizokuwa zimefichwa kisiwani Pemba.

Alisema kuwa Dk Mwinyi ni kiongozi mbunifu ambapo ubunifu wake huo umeonekana katika kampeni zake ambazo zilikuwa za kisayansi na alikutana na makundi mbalimbali na kuzungumza nayo.

Rais wa Zanzibar alimteuwa Khatib kuwa mjumbe wa baraza la wawakilishi kupitia nafasi kumi za uteuzi wa rais kwa mujibu wa katiba ya Zanzibar.

Waziri Mkuu,  Kassim Majaliwa leo amekagua kitalu cha ...

foto
Mwandishi: Khatib Suleiman, Zanzibar

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi